Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhusiano ulipo kati ya Saratani ya tezi dume na nguvu za kiume

NGUVU ZA KIUME.png Uhusiano ulipo kati ya Saratani ya tezi dume na nguvu za kiume

Fri, 18 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Korodani ni mojawapo ya sababu za kawaida zinazosababisha saratani kwa wanaume.

Korodani inapatikana chini ya kibofu cha mkojo na kazi yake ya kawaida ni kutengeneza majimaji ambayo ni sehemu ya mbegu za kiume za uzazi.

Majimaji haya ni muhimu kwa ajili ya ukuaji mbegu za uzazi za kiume.

Korodani ya saratani ni moja ya saratani zinazowapata zaidi wanaume kote duniani.

Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa, iliyotolewa mwezi Machi, 2022, Saratani kwa ujumla ni ugonjwa unaoongoza duniani kwa kusababisha idadi kubwa ya vifo, huku watu milioni 10 wakifariki kutokana na saratani mwaka 2022. Hii ni sawa na kifo kimoja kati ya vifo sita.

Kulingana na ripoti hiyo watu milioni 1.41 walifariki kutokana na saratani ya korodani.

Kwa mfano nchini Marekani taasisi ya kukabiliana na saratani -American Cancer Society (ACS) inakadiria kuwa wanaume wapya 268,490, watakuwa wamepatikana na saratani hii katika mwaka 2022. Saratani ya korodani inatokeaje?

Saratani ya Korodani hutokea pale ukuaji wa seli zisizo za kawaida unapojitokeza katika tezi ya korodani na hili ambao hutokea kwa wanaume pekee.

Kwa kawaida homoni za testosterone hudhibiti utendaji wa korodani, tezi ya prostate hutengeneza majimaji , yanayofahamika kama semen kwa lugha ya kitaamu.

Semen huwa ni mbegu za kiume za uzazi ambazo hutoka nje kupitia mrija wa mkono wakati mwanaume anapomaliza tendo la kujamiiana.

Wakati ukuaji usio wa wa kawaida wa tezi ndani ya korodani unapotokea, ukuaji wa seli mbaya pia huongezeka – na hii huitwa uvimbe – hutokea katika korodani.

Kwasababu saratani hutengenezwa na seli kutoka katika korodani, huitwa saratani ya korodani.

Saratani hii inaweza kusambaa kwenye maeneo mengine ya mwili . Kwanini ni muhimu kugundua saratani ya korodani mapema?

Dkt Afred Karagu anasema, saratani ya korodani ni mojawapo ya saratani zinazowapata wanaume zaidi, lakini ni pia ni saratani inayoweza kupona iwapo itagundulika mapema.

Dkt. Karagu kutoka Rwanda anasema njia mojawapo ya njia bora zaidi za kugundua saratani hata kabla ya dalili yoyote kujitokeza ni kwenda kufanyiwa uchunguzi.

‘’Kadri inavyogundulika mapema kuwa una saratani ya Korodani , ndivyo inavyoweza kuwa rahisi kutibika.’’, anasema Dkt Karagu.

Anasema Saratani ya korodani ina uwezekano mkubwa wa kutibiwa na ikapona kabisa iwapo itagundulika mapema.

Hatahivyo anatahadharisha kuwa ‘’Saratani ya korodani inapochelewa kugundulika, inaweza kuwa imesambaa kwenye maeneo mengine ya mwili au viungo vingine vya mbali vya mwili. Inapokuwa hivyo huenda isitibike...ndio maana tunahimiza kuwa wanaume watu wazima ni vyema wakafanya uchunguzi wa mara kwa mara wa afya zao , ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa saratani ya korodani. ‘’ anasema.

Saratani ya korodani pia imewekwa katika makundi mawili kulingana na kasi ya ukuaji wake:

Saratani ya korodani inayokua kwa kasi (aggressive) Saratani ya korodani isiyokuwa haraka- (nonaggressive)

Je saratani ya korodani inahusiana na tendo la ngono?

Daktari Karagu anasema saratani ya korodani haihusiani na tendo la ngono au la ndoa ''Kuna hizi imani ambazo sio za kweli kwamba watu wakifanya tendo la ngono sana hawawezi kupata saratani ya korodani...hilo si kweli au unapofanya tendo hilo kila mara unaweza kupata saratani ya korodani, hizi imani sio za kwali '', ameiambia BBC

Aina ya saratani ya korodani isiyokuwa haraka, uvimbe wake hukua taratibu hatahivyo, saratani ya korodani inayokua kwa kasi, uvimbe wake hukua kwa kasi, ambapo inaweza kukua kupita kiasi na kusambaa katika maeno mengine ya mwili , kama vile kwenye mifupa hali inayojulikana kama saratani ya metastatic Je ni ni zipi dalili za saratani ya korodani?

Kulingana na Dkt Karagu, zipo dalili mbali mbali za saratani ya Korodani miongoni mwake ikiwa ni pamoja na:

Kuhisi ugumu katika kukojoa Damu katika mkojo Upungufu wa nguvu za kiume Maumivu ya mifupa Maumivu ya tumbo Kupungua kwa uzito wa mwili

Nani anaweza kupatikana na saratani ya korodani?

Mwanaume mwenye umri wa kuanzia miaka 40 anatakiwa kufanya uchunguzi wa afya yake wa mara kwa mara, ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa saratani ya korodani, anasema Dkt. Karagu.

Hatahivyo anashauri kuwa wanaume wenye umri wa kuanzia miaka 50 wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kupatwa na saratani ya Korodani hivyo basi wanashauriwa kuhakikisha wanapimwa hali hii.

Ni nani hasa anaweza kupatwa na saratani ya korodani?:

Wanaume wenye umri wa kuanzia miaka 50 Watu wenye asili ya Kiafrika Iwapo historia ya familia inaonya kuwa na watu wenye saratani ya korodani Uzito wa mwili wa kupindukia Unywaji wa pombe wa kupindukia Ulaji wa nyama nyekundu Ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi

Je kuzuia saratani ya korodani inawezekana?

Daktari Leo Ngeruka kutoka Rwanda anasema mambo yafuatayo yanaweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kupata saratani hatari ya korodani

Imarisha uzito wa mwili unaofaa kwa afya yako Fanya mazoezi ya mara kwa mara Kula chakula cha afya kila wakati – matunda zaidi na mboga, na upunguze nyama nyekundu na mafuta Muone daktari wako kila mwaka ufanyiwe uchunguzi hususan kama una umri wa zaidi ya miaka 40

Chanzo: www.tanzaniaweb.live