Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhusiano kati ya Damu na Tabia

58461 Pic+uhusiano

Mon, 20 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Je, unajua kuwa tabia ulizonazo ni kutokana na kundi lako la damu? Kwa kawaida kila binadamu yuko kwenye kundi mojawapo la damu kati ya makundi manne A,B,AB na O. Makundi haya yanaweza kutumika kufahamu tabia za binadamu na jinsi hii yaweza kuwa rahisi na ya karibu zaidi kuliko kutumia nyota “astrology” kama ambavyo wengi wanafanya, na wataalamu wanasema tabia kwa uhusiano na kundi la damu ina uhakika zaidi kuliko vyanzo vingine.

Mbali na tabia, ukweli ni kwamba makundi yetu ya damu yanaweza kutuonyesha pia vile mtu anavyopendelea na asivyopendelea, kazi anazopendelea, watu anaowapendelea na hata vyakula.

Kundi la damu aina ya O

Hawa mara nyingi wanajitahidi kuwa mahodari na mashujaa katika mambo tofauti. Mara zote kiu yao ni kuwafurahisha na kuwapendeza watu wengine, ni wenye moyo wa uongozi wenye kiu ya kuwaona rafiki zao wakiwa wenye furaha wakati wote.

Si wagumu wa mabadiliko, wako tayari kubadilika, ni wenye mawazo mapana na ya wazi, si wagumu kifikra na ni marafiki wazuri.

Faida zao

Pia Soma

Ni wenye ujasiri, wanashindana katika mambo mengi mfano mambo ya maendeleo, hufanya kazi sana na kwa bidi, ni waaminifu, wanaweza kujieleza, ni marafiki wazuri, wanasamehe, mitazamo yao ni chanya, huweza kuhisi au kuona mambo hata kabla hayajatokea, wana kiu ya kufahamu na kudadisi na pia ni watu wema na watoaji.

Mapungufu yao

Mara nyingine wanaweza kuwa wenye fujo, wanaopenda sifa, wanavutia vitu upande wao, wanaepuka au kukwepa majukumu, unaweza kuona hawa wanaigiza mambo, wakitaka wametaka hadi wapate na ni rahisi kuwaondoa kwenye kile wanachokifanya “easy to be distracted”.

Maisha ya kijamii

Ni marafiki wazuri na unaoweza kuwategemea, ni waaminifu, ni wawazi, ingawa mara nyingine wanaweza kukuudhi, pia wakati mwingine wanatamani kusikilizwa wao tu.

Kazini

Wana kiu ya mafanikio, hufanya kazi kwa bidii ingawa kukatishwa tamaa na kupoteza hamasa ya kazi kirahisi sana. Mara nyingine ili wafikie malengo ni vema wakisimamiwa kwenye kazi wanayofanya badala ya kuachwa wafanye wenyewe.

Mahusiano ya mapenzi

Ni watu wanaoweza kuonyesha mapenzi kwa wale wanaowapenda ila ni vema ukafahamu kuwa watu hawa hutarajia upendo wa jinsi ile ile wao wanavyoonyesha upendo kwako bila hivyo utakosana nao.

Ukweli wa kitafiti kuhusu watu hawa

Wanaaminika huwa na tabia za kijeshi. Wengi wao kwa asili ni watu wa kupenda michezo. Wanaaminika kuwa watu wema na walio tayari kusaidia mtu yeyote, hata katika uchangiaji wa damu ‘watu wa kundi ‘O’, wanaweza kumpa damu mtu mwingine yeyote. Wanapendelea na kujisikia raha wanapokula nyama.

Chanzo: mwananchi.co.tz