Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uhusiano Kati Ya Kitambi Na Tatizo La Ukosefu Wa Nguvu Za Kiume

Kitambiz Chama Hesabu Zake Ni Makombe

Mon, 17 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna andiko linasema “ ASIYE FANYA KAZI NA ASILE “ Msingi wa andiko hili ni kupromote spirit ya kujishughulisha na ku discourage spirit ya uvivu “iddleness” katika jamii. Hata hivyo andiko hilo linaweza kuwa na maana nyingine ya ziada. Maana hii ya ziada ni tafsiri yangu binafsi kulingana na muktadha wa makala hii ya leo. Maana hii ya ziada ndio msingi wa mada yetu hii ya leo.

Kama nilivyo dokeza hapo juu, andiko asiye fanya kazi na asile linaweza kuwa na maana nyingine ya ziada ambayo kimsingi haitofautiani sana na maana ya msingi ya andiko lenyewe.

Maana hii inaweza kuwa “ ASIYE USHUGHULISHA MWILI WAKE NA ASILE CHAKULA “ kwa sababu mtu akila chakula bila kuushughulisha mwili wake chakula hicho kitaenda kubadilika na kuwa sumu ambayo itaenda kumdhuru mtu huyo, madhara yanayo weza kuyaweka maisha ya mtu huyo hatarini.

Ni nani asie jua kwamba kutofanya mazoezi ya mwili ni moja kati ya vyanzo vikuu vya matatizo mbalimbali ya kiafya kama vile kuwa na kiasi kikubwa cha mafuta yasiyo faa kwenye damu “ kolestrol ” au kuwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu.

Ni nani asie fahamu kwamba kutofanya mazoezi ya mwili ni moja kati ya vyanzo vikuu vya tatizo la kitambi, tatizo la kuwa na unene ulio pitiliza ama tatizo la kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi ?

Ni nani asie jua kuwa moja kati ya mambo yanayo weza kumuweka mtu katika hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo ni tabia ya kutofanya mazoezi ya mwili “ physical exercises “?

Ndio maanatukaambiwa asiye fanya kazi na asile. Kazi inayo zungumziwa hapa kwa tafsiri yangu (BINAFSI ) ya pili, ni shughuli yoyote ambayo inaushughulisha mwili kiasi cha kuufanya mwili utokwe na jasho jingi.

Ndio maana wataalamu wa afya duniani kote wanashauri kwamba binadamu anatakiwa kufanya mazoezi ya mwili wake “ physical exercises “ angalau mara mbili au tatu kwa wiki.

Kama ilivyo kula chakula, kufanya mazoezi ya mwili ni jambo la lazima. Kila mtu anatakiwa kufanya mazoezi ya mwili wake. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu alivyo u design mwili wa mwanadamu.

Kwa jinsi Mwenyezi Mungu alivyo u design mwili wa mwanadamu ni lazima mwanadamu awe ana ushughulisha mwili wake kila siku ili mwanadamu huyo awe na uhakika wa kuwa na afya njema na kuendelea kuwa na afya njema.

Tatizo ni kwamba watu wengi wanapo kuwa wakisikia kuhusu ishu ya kufanya mazoezi, mawazo yao huwapeleka kwenye kitu kama mazoezi ya kwenda gym kila siku, au kucheza mpira au kukimbia umbali mrefu au kuruka kamba , au kupiga push up nyingi na mazoezi yanayo fanana na hayo.

Mwisho wa siku watu hawa hukata tama hata kabla ya kuanza mazoezi hayo pengine kutokana na ugumu wa ratiba ya mazoezi ( Mtu anashindwa kubalance muda wa kwenda kazini na muda wa kwenda gym )

Mfano mtu anaishi Tegeta anafanya kazi Posta, gym ipo Mlimani City au Upanga au Masaki. Ofisini anaingia saa mbili anatoka saa kumi, muda wa gym ni kuanzia saa kumi kamili jioni.

Mwisho wa siku mhusika hata kama ana nia ya kwenda gym anajikuta anashindwa kutokana na muingiliano kati ya muda wa kuingia ofisini, muda wa kwenda gym na issue ya geographical location.

Aliwahi kusema Mchekeshaji kutoka Uganda aitwane Kansiime kwamba “ Three days after I started going to the gym, instead of losing weight, I lost morale “ akimaanisha kwamba “ Siku tatu baada ya kuanza kwenda gym, badala ya kupoteza/kupunguza uzito, nikapoteza ari ya kufanya mazoezi. A lot of people can relate with what Kansiime has just joked.

Sasa basi ninapo sema kwamba Mwenyezi Mungu alivyo u design mwili wa mwanadamu ali udesign katika jinsi na namna ya kwamba ili mwanadamu awe na uhakika wa kuwa na afya njema na kuendelea kuwa na afya njema ni lazima mwanadamu huyo awe anafanya mazoezi, simaanishi kwamba mazoezi hayo ni mazoezi ya gym, kukimbia, kucheza mpira, kuogelea, kupiga push up, nakadhalika .

Isipokuwa Mazoezi ninayo yazungumzia hapa ni ni MAZOEZI YA KUTEMBEA. Tafiti za kisayansi duniani kote zime thibitisha kwamba mazoezi ya kutembea ndio mazoezi bora kuliko mazoezi yoyote yale duniani.

Ndio mazoezi yenye faida nyingi katika afya ya mwanadamu pengine kuliko mazoezi mengine yoyote duniani.

Ninapo andika maneno haya simaanishi kwamba kwenda gym, kukimbia, kucheza mpira , kupiga push up nakadhalika ni kitu kibaya la hasha, wewe unae weza kwenda gym endelea kwenda gym, wewe unae weza kufanya mazoezi ya kukimbia, kuruka kamba, kupiga push up, kuogelea nakadhalika endelea kufanya mazoezi yako kwa kadri utakavyo ona inafaa.

Hapa ninazungumza na wewe ambae hauwezi kwenda gym, hauwezi kuogelea , hauwezi kupiga push up, hauwezi kufanya mazoezi ya kukimbia umbali mrefu nakadhalika kwamba usiwe na wasi wasi kabisa kwa sababu unaweza kupata faida nyingi na kubwa sana kwa kufanya mazoezi ya kutembea.

Bila shaka mazoezi ya kutembea ndio mazoezi yaliyo kusudiwa na Mwenyezi Mungu kwa sababu ni mazoezi yanayo weza kufanywa na kila mwanadamu na ni mazoezi ya lazima kwa sababu Mwenyezi Mungu kabla hajamuumba mwanadamu alijua kwamba mwanadamu atahitaji kutembea kila siku ndio maana akayafanya mazoezi ya kutembea kuwa yenye faida nyingi kwenye afya ya mwanadamu.

RIPOTI ZA KITAALAMU DUNIANI ZIMETHIBITISHA KWAMBA, KWENYE NYAYO ZA MIGUU YA MWANADAMU KUNA POINTS AMBAZO ZINA CONNECT NYAYO NA OGANI MUHIMU KWENYE MWILI WA BINADAMU KAMA VILE MOYO. NAAM KWENYE NYAYO ZAKO KUNA POINT AMBAZO ZINA CONNECTION YA MOJA KWA MOJA NA MOYO. MOYO NDIO OGANI MUHIMU KULIKO ZOTE KATIKA MWILI WA BINADAMU. UNAPOKUWA UNATEMBEA, KUPITIA FRICTION AMA MSUGUANO AMA MGUSANO KATI YA MIGUU YAKO NA ARDHI, FRICTION HIYO AU MSUGUANO HUO UNA IMARISHA MISHIPA NA MISULI YA MOYO NA KUUFANYA MOYO WAKO KUWA IMARA ZAIDI.

Yaani unapokuwa unatembea kwa sababu kwenye nyayo za miguu yako kuna points ambazo zina connection na moyo wako, ile friction kati ya point hizo kwenye miguu yako na ardhi inasaidia kustrengthen ama kuimarisha misuli ya moyo. Ndio maana wanasayansi duniani wanayataja mazoezi ya kutembea kama moja kati mambo muhimu sana katika afya ya moyo wa mwanadamu.

Kadri unafanya mazoezi ya kutembea kwa muda mrefu ndivyo una vyo uimarisha hata moyo wako. Mbali na kuwa na point kwenye nyayo za miguu yako ambazo zina connection ya moja kwa moja na moyo, mazoezi ya kutembea husaidia pia kuunguza mafuta yasiyo faa pamoja na sumu mbalimbali kwenye mishipa ya damu. Mafuta yasiyo faa yaliyopo kwenye mishipa ya damu yasipo shughuliwa yanaweza kuleta madhara makubwa ya kiafya kama vile shinikizo la juu la damu ambalo mwisho wa siku hu uathiri moyo pia.

Hivyo mbali na uwepo w connection kati ya nyayo za miguu ya mishipa ya moyo, mazoezi ya kutembea husaidia kuunguza mafuta yasiyo kwenye damu ambayo automatically jambo hili huenda kuunufaisha moyo.

Hiyo connection kwenye nyayo za miguu kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu haipo kati ya nyayo za miguu na moyo bali ipo pia baina ya nyayo za miguu na ogani nyinginezo muhimu kwenye mwili wa binadamu .Nitaziandikia makala siku za mbeleni panapo uzima.

So ninaposema kwamba Mwenyezi Mungu alivyo udesign mwili wa mwanadamu ame udesign katika namna ambayo ili mwanadamu huyo aendelee ku survive akiwa na afya njema ni lazima awe anafanya mazoezi hicho hapo ndicho ninacho kimaanisha, na mazoezi ninayo yanzungumzia hapa ni mazoezi ya asili kabisa ambayo ni kutembea kwa miguu yako miwili.

JE! MAZOEZI YA KUTEMBEA YAFINYIKE KWA KIWANGO GANI NA KWA MUDA GANI ?

Kwanza kabisa hutakiwi hata kuyaita mazoezi ya kutembea, kwa sababu kutembea ni hitaji la msingi kabisa kwa mwanadamu yoyote Yule kama ilivyo kwa mahitaji mengineyo kama vile kunywa maji nakadhalika.

So unacho takiwa kufanya ni kulichukulia suala la kutembea umbali mrefu kama jambo la lazima katika maisha yako. Ulifanye kuwa sehemu ya maisha yako na wala usi chukulie kama unafanya mazoezi. Nasema hivi kwa sababu uzoefu unaonyesha kwamba watu wengi wanao jiwekea malengo ya kufanya mazoezi huwa hawatimizi malengo yao na sababu ni kwamba watu wengi huwa hawapendezwi na idea kwamba wanacho kifanya ni mazoezi. Kwa mfano tuchukulie kusimama kwa muda mrefu ingekuwa ni mazoezi, ukimwambia mtu asimame juani kwa muda wa dakika ishirini mfululilo linaweza kuwa zoezi gumu sana kwake, lakini mtu huyo huyo anaweza kutazama mechi ya Simba na Yanga akiwa amesimama kwa muda wa dakika tisini bila wasiwasi wowote. Kilicho kwenye akili ya mtu huyu ni kwamba anatazama mpira na sio kwamba amesimama juani kwa muda wa dakika tisini.

Vivyo hivyo kwako wewe unaetaka kuanza kufanya zoezi hili la kutembea kwa miguu. Chukulia kwamba umebadilisha ama una badilisha mfumo wa maisha yako. Badala ya kuwa unatumia muda wako mwingi kutumia usafiri wa gari kutoka point moja kwenda nyingine basi wewe uwe unatumia miguu yako mwenyewe. Gari upande tu pale unapokuwa na dharula.

Ama kwa kiwango cha kutembea na jinsi ya kutembea, wataalamu wanashauri uwe unatembea kwa umbali mrefu na uwe unatembea haraka haraka.

Kwa wewe ambae hujatembea umbali mrefu kwa muda mrefu ( kwa sababu muda mwingi unatumia usafiri wa gari ) mwanzoni inaweza kukuwia vigumu kidogo kwa sababu hujazoea, lakini amini ninacho kuambia jambo hilo litakuwa la muda mfupi sana kwani baada ya kama wiki moja hivi utazoea kabisa na usafiri wako mkuu utakuwa miguu. Gari utakuwa unatumia pale unapo kuwa una dharula au unapo kuwa unawahi mahali kama vile kwenda kazini nakadhalika. Tofauti na hapo usafiri wako utakuwa ni miguu. Ni mazoezi ambayo uyatapenda sana kwa sababu utaona mabadiliko makubwa sana kwenye mwili wako na hutopenda urudi tena kule ulipo kuwa kabla ya kuanza kufanya mazoezi haya. Kuna watu wamekuwa addicted na mazoezi ya kutembea kiasi kwamba safari zote wanazo zifanya katika mizunguko yao ya kila siku wao hutembea tu.

Kuna watu wanaishi Makumbusho wanafanya shughuli zao posta na kila siku wanaenda kwa kutembea na kurudi wanarudi kwa kutembea. Shuhuda ninazo nyingi sana, katika makala zangu zinazo kuja nitakuwa nina andika kuhusu shuhuda za watu mbalimbali ambao wamechagua mazoezi ya kutembea kuwa sehemu ya maisha yao pamoja na faida kubwa katika afya zao ambazo wamezipata kwa mazoezi ya kutembea.

UHUSIANO KATI YA TATIZO LA KITAMBI, UNENE & UZITO ULIO ZIDI NA TATIZO LA UKOSEFU NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.

· Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya tatizo la kiriba tumbo ( kitambi ) na tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume

· Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya tatizo la kuwa na unene ulio pitiliza na tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume

· Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya tatizo la kuwa na uzito mkubwa kupita kawaida na tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume

· Kuwa na kitambi, unene ulio pitiliza na uzito mkubwa kupita kiasi tafsiri yake ni kwamba mwili mwako unakupa taarifa kwamba kuna kitu hakipo sawa ndani yako.

· Mwili wako unakupa taarifa kwamba una kiwango kikubwa cha mafuta yasiyo faa ( lehemu/kolestrol) kwenye damu yako.

· Mwili wako unakupa taarifa kwamba una kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu yako.

· Mwili wako unakupa taarifa kwamba baadhi ya ogani muhimu ndani ya mwili wako zinaogelea kwenye mafuta yasiyo faa.

· Mwili wako unakupa taarifa kwamba moyo wako umelemewa na kazi ya kusukuma damu, kwa sababu una kiwango kikubwa sana cha mafuta kwenye damu, ambacho kimeifanya damu yako kuwa nzito kupita kawaida, uzito ambao misuli ya moyo wako haiwezi kuustahimili, kwa sababu moyo umekuwa desgined kusukuma damu ambayo haina kiwango kikubwa cha mafuta , sasa kwa sababu una kiwango kikubwa cha mafuta kwenye damu basi maana yake ni kwamba moyo unafanya kazi isivyo kawaida, unatumia nguvu nyingi kusukuma damu, jambo ambalo ni hatari sana kwa afya yako kwa sababu huathiri utendaji kazi wa mishipa ya moyo wako na kukuweka katika hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo. Ndio maana wewe mwenye tatizo la kitambi, unene ulio pitiliza kiasi au uzito mkubwa kupita kiasi ukijaribu kukimbia kwa nguvu unachoka haraka na mapigo ya moyo yanaenda kasi sana na endapo utajilazimisha sana unaweza kupatwa na shambulio la moyo, kwa sababu moyo wako hauna uwezo wa kusukuma damu kwa kasi kwa sababu damu yako ina mafuta mengi sasa unapo kimbia una ulazimisha moyo wako kusukuma damu yenye mafuta mengi kwa haraka kinyume na uwezo wa mishipa ya moyo wako katika kusukuma damu.

· Mwili wako una kutahadharisha kuhusu hatari inayo weza kutokea mbele yako endapo hauta chukua hatua za haraka kukabiliana ama kudhibiti tatizo hilo.

· Mwili wako unakupa taarifa kwamba upo katika hatari ya kukabiliwa na magonjwa hatarishi kama vile presha, kiharusi, na magonjwa mengineyo ya moyo.

· Kwa hiyo mwili wako unakutaka kuchukua hatua za haraka kukabiliana na hatari hiyo kabla haijawa kubwa zaidi

JINSI KITAMBI KINAVYO PATIKANA

Kitambi ni ile hali ya tumbo kuwa kubwa na kuchomoza kwa mbele na wakati mwingine kufikia hatua ya kunin’ginia.

JINSI KITAMBI KINAVYO PATIKANA

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu, mwili wa binadamu una seli kati ya bilioni 50 hadi 200 za mafuta zilizogawanyika katika sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu.

Kwa wanawake seli hizo zipo sana katika maeneo ya matiti, kwenye nyonga, kiunoni na kwenye makalio.

Kwa upande wa wanaume seli hizo zinapatikana sana kwenye kifua, tumboni na kwenye makalio pia.

Mafuta ya tumbo yanayofanya kitambi hukusanywa kwa njia kuu mbili:

i. Njia ya kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi

ii. Na njia ya pili ni kutoka kwenye ogani za ndani kama moyo, kongosho n.k

SABABU ZA KUPATA KITAMBI

Sababu kubwa ya kitambi ni kukosekana ulingano wa nguvu(kalori) katika mwili wa mwanadamu, hali inayo sababishwa na mtu kula vyakula vinavyotia nguvu sana kuliko jinsi anavyoweza kutumia na kutoa kama taka mwili.

VYAKULA VINAVYO CHANGIA KULETA KITAMBI

Vyakula vinavyochangia kuleta kitambi ni pamoja na :

i. Vyakula vyenye mafuta mengi kama vile nyama nyekundu (iwe ni ya kuchemsha, kukaanga au kuchoma), nyama ya kuku wa kizungu ( iwe ya kuchemsha, kukaanga ama kuchoma ), mafuta ya kupikia, (hasa yale yatokanayo na bidhaa za wanyama, kama siagi, na jibini), viazi vya kukaanga kwa mafuta (chips) pamoja na pizza.

ii. Vyakula vyenye wanga mwingi kama vile ugali wa mahindi, mihogo, wali, mkate mweupe.

iii. Vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi iliyo ongezwa

( added sugar ), kama vile soda na keki.

iv. Vyakula vilivyo tengenezwa kwa ngano na sukari kama vile keki, skonzi, chapatti, maandazi, mkate mweupe nakadhalika

v. Pamoja na vinywaji vilivyo tengenezwa kwa kutumia ngano kama vile bia za aina mbalimbali na kadhalika.

Vyakula vilivyo tajwa hapo juu, vikitumiwa bila kuzingatia kanuni za mlo kamili, huchangia kuleta tatizo la kitambi.

vi. Sababu nyingine ni kutofanya mazoezi ya mwili na viungo

( physical exercises ) kwa muda mrefu.

JINSI YA KUJUA KAMA UNA KITAMBI

Kitambi kinaweza kuonekana kirahisi kwa macho. Ila kujua ni kwa kiwango gani kitambi chako kipo inabidi kufanya vipimo vya kiuno(waist) na nyonga (hips).

Mzingo wa kiuno ukiwa >102 cm au 40 kwa wanaume na >88 cm au 35 kwa wanawake, na uwiano wa kiuno na hips(Waist-Hip Ratio) ikiwa >0.9 kwa wanaume na >0.85 kwa wanawake.

BMI ya 30 au zaidi inaashiria 'Obese' uzito kuzidi kiasi. Kuwa na mzingo uliozidi kawaida ni kiashiria hatari cha matatizo ya kimetaboliki, kuliko hata cha BMI.

Kipimo kingine cha kitambi ambacho kimeonyesha uwezo zaidi kuliko BMI katika kutabiri uwezekano mkubwa wa magonjwa ya moyo ni Index Of Central Obesity(Waist-To-Height Ratio-WHtR) ambapo uwiano ukiwa sawa na 0.5 au zaidi, hii ikimaanisha mzingo wa kiuno angalau ni nusu ya kimo cha mtu.

Kipimo kingine ni Body Volume Index, kinachopima kitambi kwa kupima umbo la mtu na mgawanyo wa uzito wake.

MAMBO YANAYO MUWEKA MTU KATIKA HATARI YA KUPATWA NA KITAMBI

Tumekwisha ona hapo juu jinsi kitambi kinavyo patikana na vyakula pamoja na sababu nyinginezo zinazo sababisha kutokea kwa kitambi, sasa tutazame mambo yatakayo kufanya uwe katika hatari ya kupatwa na kitambi.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu, mambo yafuatayo huwaweka watu katika hatari kubwa ya kupatwa na kitambi :

1. Ulaji mbovu wa chakula; Ulaji mbovu wa chakula ni ulaji usio zingatia kanuni za mlo kamili. Hapa mtu hufululiza kutumia chakula cha aina fulani pekee bila kuzingatia aina nyinginezo za chakula. Mfano; mtu anaweza kuwa anakula mlo ufuatao :

Asubuhi : Mchemsho ama supu ya ng’ombe , chapatti tatu na soda moja. Mchana : Ugali nyama choma anashushia kwa maji na soda.

Jioni : Mchemsho wa kuku na bia mbili nakuendelea.

Usiku : Chips mayai au chips kuku au chips mishikaki na bia.

Mtu huyu akiendelea na utaratibu huu kwa muda mrefu, ni lazima atapatwa na kitambi.

2. Ulaji mfululizo wa vyakula vyenye mafuta mengi

3. Ulaji mfululizo wa vyakula vyenye wanga mwingi .

4. Ulaji mfululizo wa vyakula vyenye sukari iliyo ongezwa ( added sugar ).

5. Ulaji mfululizo wa vyakula vya ngano.

6. Ulaji mfululizo wa vinywaji vyenye ngano na sukari.

7. Kutofanya mazoezi ya mwili na viungo ( physical exercises ).

Mhusika anapokuwa katika makundi yote yali yotajwa hapo juu, hali huwa mbaya zaidi.

NJIA ZA KUONDOA KITAMBI

Kuwa na kitambi ni lugha ya mwili ( body-language ) inayo leta ujumbe kwako kwamba “ Mwili wako haupo salama tena “

Kama una kitambi maana yake una mafuta yasiyo hitajika mwilini, mwili wako unatumika kuhifadhi mafuta usiyo yahitaji.

Hali hii kitabibu imaanisha kwamba, ogani nyinginezo zilizomo ndani ya mwili wako zinao gelea kwenye mafuta( fats ) yasiyo hitajika yaliyomo ndani ya mwili wako, jambo linalo kuweka katika hatari kubwa sana ya kushambuliwa na magonjwa hatari kama vile shinikizo kubwa la damu, kiharusi na kisukari na kwa kutaja machache.

Hivyo basi ili kuondokana na hatari hiyo, yakupasa kupambana kuondoa hayo mafuta yasiyo hitajika mwilini mwako.

NJIA ZA KUONDOA KITAMBI.

Unaweza kuondokana na kitambi kwa kufanya diet pamoja na mazoezi ya mwili na viungo.

Vilevile unaweza kuondoa kitambi na kupunguza mafuta mwilini kwa kutumia dawa asilia ya kuondoa kitambi na kuondoa mafuta yasiyo hitajika mwilini.

JINSI TIBA YA KUONDOA KITAMBI INAVYO FANYA KAZI

1. Kuyeyusha mafuta yasiyo hitajika mwilini.

2. Kusaidia kupunguza hamu ya chakula.

3. Kuzuia kutengenezwa kwa seli za mafuta ( fat cells ) katika mwili wa mwanadamu. Unapokula chakula chenye mafuta mengi, dawa hufanya kazi ya kupambana kuyafanya mafuta hayo yasitengeneze seli za mafuta mwilini mwako. Hali hii huuepusha mwili wako kuhifadhi mafuta yasiyo hitajika mwilini.

4. Kusaidia kupunguza uzito wa mwili kwa haraka

UHUSIANO KATI YA KITAMBI NA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME

Ili uume wa mwanaume uweze kusimama barabara kitu cha kwanza kabisa mwanaume huyo lazima apate wazo la kufanya tendo la ndoa, wazo hili huweza kuchagizwa na vichocheo mbalimbali kama vile kuyaona maumbile ya mwanamke ampendae, wazo hili hunaswa kama sumaku kwenye mishipa ya fahamu iliyopo kwenye ubongo. Mishipa ya fahamu ikisha pata picha hii hutoa ishara kwenye mishipa ya fahamu iliyopo kwenye ubongo ambayo nayo hupeleka taarifa kwenye mishipa ya ateri, mishipa ya ateri ikipokea taarifa hii hufunguka na inapofunguka damu hutiririka kuelekea kwenye misuli ya uume na mwisho wa siku uume usimama.

Jambo hili ni gumu sana kwa mwanaume mwenye tatizo la kitambi, au tatizo la unene ulizo zidi au tatizo la uzito ulio pita kiasi kwa sababu zifuatazo:

1. Kwanza mwanaume mwenye kitambi, unene ulio zidi au uzito ulio zidi ana kiwango kikubwa sana cha mafuta yasiyo faa kwenye damu. Mafuta hayo kwanza huathiri utendaji kazi wa moyo katika kusukuma damu lakini pili huathiri utiririkaji wa damu kutoka kwenye moyo kuelekea katika maeneo mengine ya mwili ikiwamo misuli ya uume.. Kwa hiyo mwanaume huyu hata mishipa ya ubongo wake ikipata w azo la kufanya tendo la ndoa, damu hushindwa kutiririka vizuri kwa sababu inapata upinzani kutoka kwenye mafuta yaliyo ganda kwenye mishipa ya damu, mwisho wa siku mwanaume huyu anakuwa na weak erection na hata inapotokea mwanaume huyu akapata erection hufika kileleni kwa muda mfupi na hukosa uwezo wa kurudia tendo la ndoa.

2. Pili mwanaume mwenye kitambi, unene ulio zidi au uzito ulio zidi huweza kuwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu. Kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu huweza kuathiri utendaji kazi wa mishipa ya fahamu katika ubongo. Na kama nilivyo sema hapo awali kwamba ili uume wa mwanaume uweze kusimama ni lazima kwanza mwanaume huyo apate wazo la kufanya tendo la ndoa. Sasa basi kwa kuwa ufanisi wa mishipa yake ya fahamu katika ubongo umekuwa dhaifu , mwanaume huyu hata anapo pata wazo la kufanya tendo la ndoa, mishipa yake katika ubongo hufanya kazi katika hali dhaifu na matokeo yake hata erection yake huwa dhaifu. Kama hiyo haitoshi kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu pia huathiri utiririkaji wa damu.

3. Mwanaume mwenye kitambi, unene na/au uzito ulio zidi anaweza kuwa na kiwango kikubwa cha sumu kwenye damu, sumu ambayo huathiri suala zima la utiririkaji wa damu

SULUHISHO KWA MWANAUME MWENYE KITAMBI AMBAE ANASUMBULIWA NA TATIZO LA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME.

Mwanaume mwenye tatizo la kitambi au unene ulio zidi au uzito ulio zidi anatakiwa apate tiba ya asili ambayo kwanza itaondoa mafuta yote yasiyo faa kwenye mishipa ya damu, tiba itakayo rekebisha kiwango cha sukari kweny e damu yake, tiba ya asili itakayo ondoa sumu yote kwenye damu yake. Tiba zote hizi kwanza zitaondoa kabisa kitambi alicho nacho, pili zitapunguza unene alionao , tatu zitapunguza uzito wake kwa kiasi kikubwa sana na mwisho zita mtibu na kumponyesha kabisa tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume linalo mkabili.

MAKALA HAYA YAMEANDALIWA NA DUKA LA KUUZA DAWA LA NEEMA HERBALIST. TUNAUZA DAWA MBALIMBALI ZA ASILI AMBAZO ZINATIBU NA KUPONYESHAMATATIZIO TUNAPATIKANA UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM, NYUMA YA JENGO LA UBUNGO PLAZA JIRANI NA SHULE YA MSINGI UBUNGO NATIONAL HOUSING.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live