Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ugonjwa wa surua wazidi kuwa tishio duniani

Thu, 15 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geneva, Uswizi. Shirika la Afya duniani (WHO), limesema kuwa maambukizi ya ugonjwa wa surua yameongezeka mara tatu katika kipindi cha miezi saba ya mwaka 2019.

Hata hivyo, shirika hilo imesema ongezeko hilo I kubwa ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka uliopita.

Shirika hilo limesema hadi sasa, maambukizi 364,808 yamekwishajitokeza mwaka huu, ikilinganishwa na visa 129,239 vilivyokuwa vimeripotiwa katika miezi saba ya mwanzo ya mwaka 2018.

Kwa mujibu wa tangazo la shirika hilo, ongezeko hilo limechangiwa na kudorora kwa shughuli za utoaji wa chanjo ya ugonjwa huo.

“Idadi kubwa ya maambukizi ya ugonjwa wa surua iliripotiwa katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Madagasca, Ukraine, Angola, Cameroon, Chad, Nigeria, Sudan na Sudan Kusini,”  lilifafanua tangazo hilo.

WHO ilisema wa upande wa bara la Afrika maambukizi  ya ugonjwa huo yameipanda kwa asilimia 900.

Pia Soma

Tangazo hilo la WHO limeipa nguvu kampeni iliyoanzishwa na Ujerumani kuweka ulazima wa kinga ya surua kwa watoto wote wa shule za chekechea na wafanyakazi kuanzia mwezi Machi mwaka ujao.

Chanzo: mwananchi.co.tz