Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ugonjwa wa kutoa harufu ya ajabu wamtesa mama huyu

Kelly White Kelly Fidoe-White

Wed, 15 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hali ya kusikitisha, mwanamama Kelly Fidoe-White (41) raia wa Uingereza amesema kila siku inamlazimu kuoga sio chini ya mara nne kwasababu amezaliwa na tatizo la kutoa harufu mbaya kama samaki aliyeoza na hali hiyo hujionesha hadi katika mkojo.

Kelly amesema alianza kujigundua kuwa ana harufu ya tofauti akiwa na miaka 6 tu lakini hakujua hasa tatizo hilo linatokana na nini hadi alipofikisha miaka 34 ndio akaelewa vizuri.

Amesema inamlazimu kuoga mara nne kwa siku na kujipulizia pafyumu/deodorant kila wakati lakini ndani ya muda mfupi tu tatizo linarudi tena. Amesema ametumia sabuni za kila aina kuogea lakini wapi sana sana mwili ukiwa katika uasili wake kidogo kuna afadhali.

Ameongeza kuwa baadhi ya watu wasiojua tatizo hilo humsema vibaya wakidhani sio msafi mara unene ndio chanzo apungue lakini anasema ukweli ni tofauti kwani alipokuwa mwembamba hali ilikuwa hivyo hivyo na pia yeye ameajiriwa sekta ya afya(radiographer) hivyo watu kudhani labda ni mchafu inamfanya ajisikie vibaya hadi kulazimika kwenda kwa wanasaikolojia na hata kazini anapendelea zaidi zamu za usiku.

Amesema akikaa karibu na watu anaonekana kama kero flani hivi. Pia kuna baadhi ya vyakula kama maini, figo, maharage, karanga etc hatakiwi kula kwani vinachochea ukubwa wa tatizo hilo na Kuna vyakula ameshauriwa ale kupunguza ukali wa tatizo.

Katika lugha rahisi tatizo hilo linajulikana kama trimethylaminuria 'Fish-Odour Syndrome' na hadi sasa rekodi za dunia zinaonesha watu 100 tu ndio wana tatizo hilo lakini wataalam wanasema kuna uwezekano wapo watu wengine kukaribia hata 200 ambao rekodi zao bado kukusanya.

Watu wenye tatizo hilo wengine hutoa harufu kama ya samaki waliooza, mayai vinza, uchadu uliooza, mkono ama kinyesi na hii husababishwa na miili yao kushindwa kutoa sumu-taka iitwayo trimethylamine.

Na inaelezwa wataalam bado hawajagundua dawa ya kuondoa au kuponesha tatizo hilo moja kwa moja. Kelly amesema ameamua kuzungumza kuhusu hali yake ilimkutoa elimu kwa wasiofahamu hali hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live