Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Afya kuhusu utata wa chanjo

VIKOU Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya

Fri, 20 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima, atolea ufafanuzi na kuweka sawa wale wanaodhani ajenda ya Uviko-19 inatofautiana kati ya awamu ya tano ya Hayati Rais Magufuli na awamu ya sita ya Rais Samia.

Amesema kuwa wananchi hawakuelewa kilichokuwa kinakataliwa katika serikali ya awamu ya tano ni kutokimbilia chanjo hizo pasipo kujiridhisha kisayansi.

"Naomba kutoa ufafanuzi , hapana, serikali ya awamu ya sita haijabadilisha muelekeo, labda wasikilizaji hawakuelewa vizuri muelekeo wa serikali ya awamu ya tano, maana serikali ya awamu ya sita imekuja kuendeleza mipango iliyoachwa na serikali ya awamu ya tano"

Tangu kuanza kwa utoaji wa Chanjo ya Uviko-19, kumekuwepo maswali mengi kwa ya Wizara ya Afya kuhusu msimamo wao juu ya chanjo hiyo. Hata hivyo Wizara hiyo inaendelea kutoa hamasa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupokea Chanjo hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live