Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uelewa wakwamisha wanaume kufanyiwa tohara

60e30de9451256ad711691850cafcd0c Uelewa wakwamisha wanaume kufanyiwa tohara

Sun, 6 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

UELEWA mdogo sambamba na kukosa ujasiri wa kufanya maamuzi bado ni sehemu ya vikwazo vinavyokwamisha kufikiwa kwa malengo ya tohara katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.

Hayo yalibainishwa na wadau mbalimbali wakiwemo watu waliojitokeza kufanyiwa tohara kwenye kampeni maalumu inayoendeshwa na Shirika la Watereed inayokwenda sambamba na Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo shirika hilo limeamua kutoa huduma hiyo katika kata zote za wilaya ya Mbarali.

Lengo la kampeni hiyo ni kuwasogezea kwa karibu wananchi elimu juu ya umuhimu wa tohara.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi,baadhi ya watu wakiwemo wenye umri mkubwa waliopata huduma ya tohara walisema awali hawakuwa na elimu lakini sasa wametambua umuhimu lakini wengine wakasema bado kuna woga ndani ya jamii.

Method Chaula mwenye umri wa miaka 58 ni mkazi katika kitongoji cha Magea katika mji mdogo wa Rujewa wilayani hapa anasema "Nimejisikia kuja kufanyiwa tohara baada ya kuona inasaidia kwa kiasi kikubwa kuepusha watu na maambukizi ya magonjwa mengi ikiwemo VVU, kaswende na magonjwa mengine mengi.”

Ibrahimu Mwandulifwa mkazi katika kijiji cha Igawa wilayani Mbarali mwnye umri 38 ni mume wa mke mmoja ambaye anasema amefikia uamuzi wa kufanyiwa tohara baada ya kupata elimu na kutambua kuwa alikuwa akifanya tendo la ndoa katika mazingira yasiyo salama kwake kutokana na kutotahiriwa.

Mtoa huduma ya tohara Anna Jackson alisema kwa asilimia 60 maambukizi ya VVU yanapunguzwa kwa wanaume kufanyiwa tohara.

"Tuko hapa kwa ajili ya kuelimisha jamii kupima VVU pamoja na kufanyiwa tohara.Walio tayari kufanyiwa tohara na tunawafanyia hapa ni walio na umri wa kuanzia miaka 15 mpaka mzee kikongwe.Na tumeona watu wana mwitikio mkubwa sana na tunaendelea kuwafanyia hapahapa kwenye gari maalumu." Alisema.

Dk Anna alisema tangu walipoanza kampeni Novemba 23, mwaka huu mpaka Desemba Mosi siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani mwitikio wa watu kujitokeza kupima VVU na kufanyiwa tohara ulikuwa ni mkubwa kwani hadi siku hiyo zaidi ya watu 100 walikuwa wamefanyiwa tohara.

Alisema mwitikio haukuishia kwa vijana pekee, kwa kuwa mpango ulilenga kuwafikia kuanzia vijana wenye umri wa miaka 15 hadi wazee vikongwe wapo pia wazee wenye umri wa miaka zaidi ya 70 walijitokea na kufanyiwa tohara.

Chanzo: habarileo.co.tz