Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ubuyu unaongeza kinga kwa kuwa na vitamin C kwa wingi

E5f336cd2d1bf218e16ce255bb942a61 Ubuyu unaongeza kinga kwa kuwa na vitamin C kwa wingi

Fri, 12 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WANANCHI wanashauriwa kula unga wa ubuyu kwani una vitamin na madini mengi kuliko matunda mengine.

Aidha unga huo unaelezwa kuwa na vitamin C nyingi mara sita zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.

Muuzaji wa bidhaa za asili za kutunza ngozi, Eunice Panga ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Paroti alisema hayo alipokuwa akizungumza na Habari Leo.

Panga ambaye alishiriki Wiki ya Viwanda ya Wanawake na Maonyesho ya Bidhaa yaliyomalizika jijini Dar es Salaam, alisema ubuyu una kiwango kingi cha madini ya calcium mara mbili zaidi ya maziwa ya ng’ombe, lakini mdini mengine yanayopatikana katika ubuyu ni madini ya chuma, magnesium na potassiamu inayopatikana katika ndizi.

Alisema ubuyu unaongeza kinga ya mwili kwa sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamin C.

Alitaja bidhaa anazouza mbali na unga wa ubuyu ni mafuta ya ubuyu, sabuni ya ubuyu, unga wa rosela pamoja na rose water kwa ajili ya kuipa ngozi unyevu.

“Utumiaji wa bidhaa hizi asili zinasaidia kutunza ngozi na maradhi mbalimbali pamoja na mionzi ya jua, kuondoa vipele na chunusi pamoja na ngozi kavu iliyokauka na kupasuka,” alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz