Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uboreshaji Hospitali ya King Feisal kukamilia mwezi ujao

De912f3fdbd74c1fd76710685b6ce387.png Uboreshaji Hospitali ya King Feisal kukamilia mwezi ujao

Tue, 26 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

UBORESHAJI wa miundombinu ya Hospitali ya King Feisal unakaribia kukamilika na mkandarasi anatarajiwa kukabidhi mradi huo mwezi ujao.

Uboreshaji huo ulianza Januari, mwaka jana na ulipangwa kukamilika mwaka jana lakini ulikwama kwa sababu ya janga la covid-19 ambalo nchi imekuwa ikipambana nalo kwa karibu mwaka mmoja sasa.

Mradi huo umehusisha ujenzi wa kituo kipya cha wagonjwa wa nje, kliniki ya huduma za malipo, ukarabati na upanuzi wa kituo cha zamani, ufungaji wa njia panda inayounganisha jengo jipya na la zamani pamoja na ununuzi wa vifaa.

Uboreshaji huo utaifanya hospitali hiyo sasa kuwa na vyumba vinne vya madaktari kutoka vyumba 20.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya King Faisal, Miliard Derbew alisema kazi hiyo ilipangwa kukamilika Juni, mwaka jana lakini janga la covid-19 na mazuio ya kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo kulisababisha kuchelewa.

“Hata baada ya kurekebishwa masharti ya mazuio, muda uliopangwa kukamilika yaani Septemba, mwaka jana haingewezekana kwani sehemu nyingine duniani zilizuiwa hivyo kukosekana vifaa vinavyohitajika kutoka nje.”

"Ingawa kufungiwa kulikuwa kumepunguzwa lakini kulikuwa na ucheleweshaji wa kuwasili kwa vifaa. Kufikia Agosti, mwaka jana ujenzi ulikuwaumrfikia karibu asilimia 60 na Desembauilikuwa karibu asilimia 90. Sasa tunatarajia kukamilisha Februari mwaka huu,” alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz