Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UTAFITI: Ujanjaujanja saluni hatari kwa afya

44628 Pic+salun UTAFITI: Ujanjaujanja saluni hatari kwa afya

Mon, 4 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Unyoaji nywele usiozingatia usalama wa afya za wateja katika saluni mbalimbali mkoani Kilimanjaro, umeibua tishio kubwa la magonjwa ya kuambukiza, hasa homa ya ini na ngozi.

Wakati wa kunyoa, mashine za umeme zinazotumika huweza kusababisha michubuko midogo kichwani, hasa kwa wanaochonga nywele na hivyo kuhitaji spiriti ili kutibu vidonda hivyo, au kuziosha mashine hizo kwa dawa hizo ili kuepuka maambukizi.

Spiriti ni dawa iliyo na mchanganyiko wa ethanol, methanol na kemikali nyingine, hutumika kuua vijidudu kama virusi na fangasi katika sehemu iliyochubuka na kupalinda na pia huweza kutumika kama dawa ya kusafishia.

Lakini pamoja na kusafishia spiriti kabla ya kunyoa na pia kuzihifadhia kwenye mashine za joto (steriliser) kwa lengo la kuua vijidudu, vinyozi wanakiuka taratibu za usafi na hivyo kuhatarisha afya za wateja.

Utafiti umebaini kuwa mashine za umeme za kunyolea nywele husafishwa kwa spiriti iliyopunguzwa uwezo wa kupambana na vijidudu hivyo, wakati nguo hazihifadhiwi sehemu zisizo rafiki kwa vijidudu na hazisafishwi kwa maji ya moto au dawa.

Mwananchi imebaini kuwa baadhi ya wahudumu wa saluni, hununua spiriti na kisha kuzichanganya na maji ili kuongeza ujazo wa spiriti, jambo ambalo hupunguza nguvu ya dawa hiyo.

Baadaye hutumia spiriti hiyo kuoshea mashine za kunyolea kuonyesha kuwa wanaua bakteria, fangasi na virusi vya magonjwa ya kuambukiza.

“Wewe nenda maeneo ya Pasua, Kiborlon, Mji mpya, Korongoni na hata hapa katikati ya mji kama utakuta wana sterilizer machine (mashine ya joto ya umeme). Hizo saluni ni za kuhesabu,” alisema mmoja wa wahudumu.

“Bakteria (wadudu) na parasites (vimelea) wanaweza kuishi siku saba au zaidi kwenye vifaa vya saluni, taulo, viti na kwenye mashine za kunyolea kama hazitasafishwa vizuri,” ilielezwa na chanzo hicho.

Mtaalamu wa masuala ya afya Hospitali ya Rufaa Mawenzi ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kama taulo zisipokaushwa vizuri, zinaweza kusababisha madhara. “Ukitizama mtu amenyolewa labda ndevu au hata nywele kichwani, anasafishwa na taulo halafu inaanikwa. Haijakauka vizuri anakuja mwingine anafutiwa, hii si sawa,” alisema mtaalamu huyo.

Utafiti uliofanywa Afrika Kusini na kuchapishwa na jarida la South Africa Medical Journal Vol 108,Na 4, umebaini baadhi ya magonjwa ya kuambukiza, kama homa ya ini, hutokana na mashine za kunyolea.

Katika utafiti huo, wanasayansi walichukua mashine za kunyolea nywele kutoka saluni 50 na kuzifanyia uchunguzi na kukuta asilimia 50 ya mashine hizo zikiwa na vijidudu vya ugonjwa wa ini (HBB).

Ingawa haikubainika uwepo wa Virusi vya Ukimwi, wateja wanaweza kuambukizwa Ukimwi kwa kuwa wakati wa kunyoa hutokea michubuko na ukweli kwamba mashine hazioshwi ipasavyo.

Wataalamu, madaktari wanena

Profesa John Shao ambaye ni mtaalamu bingwa wa microbiolojia, aliiambia Mwananchi kuwa kitaalamu ngozi ya binadamu na nywele zina vijidudu.

“Vijidudu hivi vinaweza kuambukizia watu wengine hasa watoto na vijana,” alisema Profesa Shao.



Chanzo: mwananchi.co.tz