Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UTAFITI: Mgonjwa mmoja kati ya watano wanaofanyiwa upasuaji hufariki

1194 Misuli 660x376 TZW

Sun, 7 Jan 2018 Chanzo: millardayo.com

Hatari ya kufariki Dunia kutokana na upasuaji wa kitabibu barani Afrika ni zaidi ya mara mbili ya wastani wa Kimataifa, hii ni kulingana na ripoti inayochunguza matatizo ya afya barani Afrika.

Utafiti huo umesema kuwa katika hali ya kawaida, wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji barani Afrika hawachukuliwi kuwa katika hatari ikilinganishwa na wenzao wa Mabara mengine, kwa vile wengi wao wanakuwa vijana na huwa wanafanyiwa upasuaji mdogo tu.

Watafiti wamegundua kuwa  mtu mmoja katika kila watu watano wanaofanyiwa upasuaji Afrika anapata matatizo baadae na hii ni kulingana na ripoti ya wataalmu hao, hatari inayoambatana na upasuaji uliopangwa mapema, iko katika kiwango cha asilimia moja Afrika, huku athari hiyo katika wastani wa kimataifa ni asilimia 0.5.

Uchunguzi huo uliochapishwa katika jarida la afya la The Lancet unaelezwa kuwa ndio uchunguzi mkubwa zaidi juu ya upasuaji Afrika, uliowaleta pamoja zaidi ya watafiti 30, walioangalia data kutoka hospitali 247 katika nchi 25 Afrika, lengo likiwa kufuatilia operesheni 10,885 walizofanyiwa wagonjwa.

Uchunguzi huo ulijumuisha maelezo zaidi kuhusu matatizo yaliyojitokeza, idadi ya vitanda vya kulazia wagonjwa, vyumba na vifaa vya kufanyia operesheni hizo na kupata habari muhimu juu ya miundo mbinu ya hospitali.

Zaidi ya wagonjwa wanne kwa kila wagonjwa watano ambao walichunguzwa, wangeweza kuaminiwa kuwa na hatari ndogo kwa kuzingatia kwamba wengi bado ni vijana walio katika umri wa wastani wa miaka 38, matatizo yaliyotokana maambukizi kufuatia upasuaji yaliwakumba asilimia 18.2 ya wagonjwa wote na takriban mgonjwa mmoja kati ya 10 aliyekuwa mamatatizo hayo aliaga dunia.

Mtafiti Mkuu Bruce Biccard, ambaye ni profesa katika hospitali ya Groote Schuur iliyoko mjini Cape Town, Afrika Kusini alielekeza lawama zake katika kipindi cha baada ya upasuaji ambapo asilimia 95 ya vifo hivyo hutokea.

Profesa Bruce Biccard  amesema “vifo hivi vingeweza kuepukika iwapo kungekuwepo na ufuatiliaji wa wagonjwa waliokuwa na matatizo, matokeo ya baada ya uchaguzi yataendelea kuwa mabaya barani Afrika hadi tatizo la vifaa na mazingira salama ya kufanyia kazi litakaposhughulikiwa.”

Mataifa yaliyofanyiwa uchunguzi ni pamoja na Algeria, Libyana na Misri, lakini haukujumuisha baadhi ya mataifa masikini barani Afrika kama vile Burkina Faso, Liberia na Sudan, au hata taifa linalokumbwa na vita la Somalia. Hospitali ndogo ndogo zilizoko vijijini pia hazikufanyiwa uchunguzi huu.

MAKOSA YALIYOSABABISHA MADUKA 4 YA DAWA KUFUNGIWA

MUHIMBILI HOSPITALI WAZUNGUMZIA HALI YA MZEE KINGUNGE

Chanzo: millardayo.com