Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

USAID yaipa Tanzania Dola 750,000 kupambana na COVID-19

66a61920d3cb6300568d48950c7951ce Mapambano dhidi ya Corona, USAID yatoa Dola 750,000

Sat, 11 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imesaini mkataba na Shirika la Marekani la Maendeleo la Kimataifa (USAID) wa mradi wa kuimarisha mapambano dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona nchini.

Mradi huo wa dola za Marekani 750,000 sawa na sh bilioni 1.7 za Kitanzania umesainiwa mjini Dodoma, utaelekezwa kwenye hospitali nne za rufaa za mkoa ili kuzisaidia kupambana na mlipuko wa ugonjwa huo.

Hospitali zitakazonufaika na mradi huo ni ya Rufaa Dodoma, Bombo, Mount Meru Arusha na Sekou Toure ya Mwanza

Mganga Mkuu wa Serikali, Aifello Sichalwe, amesema mradi huo mpya unakusudia kuhakikisha hospitali hizo za rufaa zinatoa huduma bora kwa wagonjwa wa Covid 19.

Alisema kupitia mradi huo hospitali hizo za rufaa zitanufaika na vifaa tiba zikiwemo mashine za oxygen za kuwasaidia kupumua wagonjwa wanaofika wakiwa kwenye hali mbaya ya kuhitaji mashine. Pia wahudumu wa afya watapewa mbinu mbalimbali za namna ya kukabiliana na ugonjwa huo.

Naye Meneja mradi kutoka USAID, Dk Miriam Kombe alisema, kupitia mradi huo utasaidia kupunguza athari za janga la Corona kwa jamii.

Alisema janga hilo la Corona limekuwa changamoto kubwa kwa usatawi wa afya, na usalama wa kiuchumi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz