Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UNFPA yasaidia mashine ya 'Utra Sound' Bariadi

8ac863172ecca29b06564ce82a2480e9 UNFPA yasaidia mashine ya 'Utra Sound' Bariadi

Wed, 23 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Hospitali ya Mji wa Bariadi-Somanda imepokea mashine ya kupimia wajawazito ‘Ultrasound’ yenye thamani ya shilingi milioni 30 kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu (UNFPA).

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga amesema kupatikana kwa kifaa hicho kitarejesha huduma za upimaji kwa akina mama wajawazito na kulishukuru shirika hilo kwa msaada huo.

Aidha, Kiswaga amewataka watumishi wa hospitali hiyo kuongeza umakini katika matumizi na utunzaji wa vifaa tiba katika hospitali hiyo ili huduma ya upimaji wa magonjwa na vitu mbalimbali vya kitiba zisiweze kusimama.

Chanzo: habarileo.co.tz