Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UNAAMBIWA: Magonjwa ya ngono ni tishio migodini!

598f215fd4a3ad27b11361d1607dfb6c Magonjwa ya ngono ni tishio migodini!

Mon, 17 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uwepo wa wimbi kubwa la maambukizi ya magonjwa ya ngono umetajwa kuwa tishio kubwa linalowakabili wachimbaji kwenye migodi iliyopo katika Kijiji cha Itumbi, Kata ya Matundasi, wilayani ChunyaM Mkoa wa Mbeya.

Kutokana na hali hiyo, wachimbaji na wakazi wa kijiji hicho wameiomba serikali na wadau wa sekta ya afya kuongeza nguvu ya utoaji huduma za matibabu ya magonjwa hayo kwenye zahanati ya kijiji hicho ili kuwanusuru.

Wachimbaji hao walisema hayo wakati wakizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimri, Prof Yunus Mgaya alipotembelea mgodi wa dhahabu wa Sipemba uliopo katika Kijiji cha Itumbi, Kata ya Matundasi, wilayani Chunya.

Walisema maambukizi ya magonjwa ya ngono ni makubwa katika kijiji hicho kutokana na kuwapo kwa muingiliano mkubwa wa watu kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo wanaofanyabiashara biashara ya ukahaba ili kujiingizia kipato.

Mmoja wa wachimbaji hao, Thomas Simon alisema kijiji cha Itumbi kina watu wengi na ugonjwa wa kisonono uko juu na vijana wengi wanaopata maambukizi hawapati tiba inayostahili kutokana na zahanati kukosa dawa.

"Tumekuwa tukipata mara kwa mara vipimo vya virisi vya ukimwi (VVU) na magonjwa mengine ya zinaa, lakini unakuta majibu yanatoka kuwa una maambukizi ya kisonono na inamlazimu daktari akuandikie dawa ukanunue dukani na maduka binafsi tunakuta bei ziko juu hivyo kijana anaamua kukaa na ugonjwa wake bila kutibiwa, sasa hii ni hatari sana," Thomas.

Wachimbaji hao wameomba wataalamu wa magonjwa ya ngono wapelekwe kijijini hapo ili kunusuru afya zao, huku pia wakiiomba NIMR kuongeza nguvu kwenye safari za kliniki inayotembea ili kutoa huduma.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Dk Daison Andrew aliwapongeza wachimbaji hao kwa kuwa wawazi kuelezea tatizo linalowasibu na kuahidi ndani ya mwezi mmoja kupeleka daktari kwenye zahanati ya kijiji hicho ili kuongeza nguvu kwa wauguzi waliopo.

"Nawapongeza kwakuwa mmekuwa wawazi, ndani ya mwezi mmoja tutaleta daktari mtaalamu pale zahanati. Muhimu tunachosisitiza ni watu kujitokeza kupima ili walio na shida watibiwe. Ukipima na kuijua afya yako utaishi kwenye uhalisia Zaidi," alisema Dk Andrew.

Kwa upande wake, Prof Mgaya alisisitiza umuhimu wa kujikinga na kutoendekeza ngono zembe kwa kufanya hivyo kunahatarisha afya ya watu kwenye migodi.

Alisema alichobaini ni kutokuwapo kwa elimu ya kujikinga na magonjwa ya zinaa kijijini hapo ndiyo sababu tatizo hilo ni kubwa.

Alishauri wadau sekta ya afya kushirikiana na wadau wa sekta ya madini kutoa elimu kwa wachimbaji hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live