Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UIaji Futari nyingi, Chanzo cha Mshtuko wa Moyo

F6ce63d0b4cb48b0ce43d42b8e2e5468 UIaji Futari nyingi, Chanzo cha Mshtuko wa Moyo

Wed, 5 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Imefahamika kuwa ulaji wa futari nyingi kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan unaweza kuwa chanzo cha wa mshtuko wa moyo.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi, amesema kula futari nyingi wakati wa Magharibi sio tu kutafanya wafungaji kuongezeka uzito, bali matatizo mbalimbali ya moyo kama shinikizo la damu la juu, moyo dhaifu, moyo uliopanuka, mishipa/mirija ya moyo iliyoziba, wanaweza kupata matatizo ya kiafya .

“Ulaji wa chakula kingi kunaweza kuchochea mstuko wa ghafla wa moyo, mshtuko wa moyo unasababisha mamilioni ya watu kupoteza maisha kila mwaka duniani.”amesema Profesa Janabi na kuongeza

“Kila mwaka vifo hivi vinaongezeka zaidi duniani kipindi hiki cha Ramadhan na wakati wa sherehe mbalimbali kama vile Krismasi, Pasaka na Mwaka mpya.” alisema

Alisema takwimu zinaonyesha magonjwa ya moyo ndio yanaongoza duniani kwa kusababisha vifo ukilinganisha na magonjwa mengine ambapo zaidi ya watu milioni 18 hufariki duniani kila mwaka kwa sababu ya magonjwa ya moyo hii ni sawa na asilimia 31 ya vifo vyote duniani.

Kati ya vifo hivyo asilimia 85 vinatokana na mstuko wa moyo, robo tatu ya vifo hivi vya moyo vinatokea kwenye nchi zenye uchumi mdogo au uchumi wa kati.

Hata hivyo amesema asilimia 80 ya magonjwa ya moyo yanaweza kuzuilika kwa kubadili mtindo wa maisha, kuacha uvutaji wa sigara, kula vyakula bora na kwa kiasi kupunguza uzito, kufanya mazoezi na kupunguza unywaji wa pombe.

Alisema tafiti zinaonyesha kipindi kama hiki cha Ramadhani vifo vinavyotokana na mstuko wa moyo huongezeka mara nne zaidi kutokana na sababu ya ulaji wa chakula kingi mpaka kuvimbiwa wakati wa kufuturu/iftar au wakati wa daku na kwamba tumbo la chakula linapanuka ili kupokea chakula hicho.

“Hii inapelekea damu mwilini kujipanga upya kwa kutoa damu nyingi kutoka kwenye moyo na kupelekwa kwenye njia ya chakula, ili kusaidia kusaga chakula kingi kilicholiwa nyakati za futari/daku.

Profesa Janabi amesema hali hiyo ikimkuta mlaji ambae ana tatizo lake la moyo au shinikizo la damu la siku nyingi kwa mfano mirija au mishipa yake ya damu ya moyo imeziba kidogo au sana huu mbadiliko wa mwendo wa damu kutoka kwenye moyo kwenda kwenye tumbo ndio unapelekea kuchochea na kusababishaa mstuko wa moyo na athari zake.

Alisema tumbo lililojaa kutokana na ulaji wa chakula kingi husababisha moyo kwenda mbio na mapigo kutokwenda sawa sawa hii pia huchochea mstuko wa moyo na wengine kupata kiarusi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz