Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

UFAFANUZI: Serikali yazungumza kuhusu aliyekutwa na kirusi cha 'Omicron'

Missiba Pic Data Aliyekutwa na ‘Omicron’ aanza kuchunguzwa

Mon, 6 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema tayari imeanza kufuatilia kupitia vyombo vya ndani taarifa za uwepo wa abiria mmoja aliyerudi nyumbani (India) mwenye aina mpya ya kirusi cha Uviko-19 ‘Omicron’ ambaye alitokea Tanzania.

Imeeleza kuwa kwa mujibu wa taarifa za Maabara Kuu ya Taifa mpaka sasa hawajabaini anuwai mpya ya Uviko-19 (Omicron).

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Abel Makubi wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu ufafanuzi wa abiria huyo na wito wa kuendelea kuchukua tahadhari.

Amesema kwa kushirikiana ubalozi wa Tanzania nchini India wanafuatilia ili kubaini ukweli wa jambo hilo na baadaye kuchukua hatua stahiki.

“Bado haijajulikana kama abiria huyu alitokea Tanzania moja kwa moja au alipita Tanzania kuelekea India. Pia haijulikania alipita wapi kabla ya kufika India,” amesema Profesa Makubi.

Amesema Maabara ya Taifa pia imekuwa ikichunguza mabadiliko ya kirusi (Gene sequencing) kwa kuangalia uwepo wa anuwahi mbali mbali zinazotokana na mabadiliko ya Uviko-19 ikiwemo anuwai mpya ya Omicron.

Advertisement Amesema maabara inao uwezo wa kubaini anuwai mpya ya Omicron na wanaendelea kuzifuatitilia sampuli zote na kwamba wakibaini uwepo wa anuwahi mpya watatoa taarifa.

“Mpaka sasa uchunguzi zaidi ya wanasayansi duniani unaendelea kujua anuai hii ya Omicron ina madhara ya kiasi gani kwa mtu anapoambukizwa na taarifa kutoka mataifa yaliyobaini wananchi wenye virusi hivi, wamekuwa na dalili za kiasi na nyepesi bila kuingia mahututi,” amesema.

Hata hivyo amesema waliobainika wengi wamechanja hivyo huenda chanjo imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza makali ya ugonjwa.

Profesa Makubi amewasihi wananchi kutokuwa na hofu kutokana na habari hiyo bali waendelee kuwa watulivu na kutekeleza shughuli za maendeleo huku wakichukua tahadhali zote ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka, kuvaa barakoa na kujiepusha na misongamano isiyokuwa ya lazima na kufuata miongozo mbalimbali inayotolewa na Wizara kupambana na Uviko-19.

Profesa Makubi amesema hatua zitaanza kuchukuliwa kubaini iwapo maeneo yanayotakiwa kuweka miundombinu ya kujikinga yanafanya hivyo.

Mapema leo, taarifa hiyo imechapishwa na vyombo vya habari vya India na kuenea katika mitandao ya kijamii ikielezwa kuwa India wamegundua abiria mmoja anayerudi nyumbani (India) mwenye virusi hivyo akitokea Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live