Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Tupambane na corona lakini tuchukue tahadhari UKIMWI upo" Ummy

NTK4C5C4PVFADEDP74JMLNE2EQ 660x400.webp "Tupambane na corona lakini tuchukue tahadhari UKIMWI upo" Ummy

Sun, 1 Aug 2021 Chanzo: millardayo.com

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu amesema wakati Serikali na Jamii ya kitanzania inaendelea kupambana na ugonjwa wa Corona lazima jamii iendelee kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa mengine ya hatarishi ukiwemo ugonjwa wa UKIMWI.

Ummy ameyasema hayo  alipokuwa anazindua uwekaji wa makasha ya kusambazia kondomu maeneo ya watu na yenye mikusanyiko ambapo ameeleza kwa kufafanua takwimu zinaonesha kuwa kwa mwaka takribani watu 72 elfu wanaambukizwa maambukizi mapya ya ugonjwa huo.

Akiendelea kufafanua kwa siku watu zaidi 200 wanapata maambukizi na kuitaka jamii kuendelea kujiepusha kujikinga na kuendelea kusikiliza maelekezo na wataalam wa Afya.

Ummy alisema jamii iache kuwa na dhana potofu ya ikimuona mtu amebeba kondomu kumuhisi ni muhuni bali jamii ijifunze kujilinda na maambukizi yatokanayo na ngono zembe ambazo zimekua zikiharibu maisha ya baadhi ya watu.

Sambamba na hilo amewaagiza watendaji wa TAMISEMI kwa kushirikiana na Tayoa kuhakikisha wanasambaza makasha hayo na kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya UKIMWI hadi maeneo ya Vijijini ambapo baadhi ya jamii haina uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa huo.

Makasha hayo tayari yamefika kwenye halmashauri 169 kati ya halmashauri 184 kwa Tanzania bara hivyo wajitahidi kufikisha maeneo mengi zaidi kuokoa taifa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabil Shekimweli akitoa wito kwa wadau wa maendeleo kuendelea kutoa elimu kwa jamii athari za ugonjwa wa UKWIMWI na kuwataka kufanya tafiti ili kujua usahihi na mahitaji.

Chanzo: millardayo.com