Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tumbaku chanzo cha saratani zote, magonjwa yasiyoambukiza

60729 Pic+tumbaku

Fri, 31 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati takwimu zikionyesha asilimia 16 ya Watanzania wanatumia tumbaku, Shirika la Afya Duniani (WHO) limebainisha kuwa waathirika wakubwa ni wanawake na watoto huku vifo vingi vitokanavyo na matumizi hayo vikitarajiwa miaka ijayo.

WHO imesema njia sahihi zisipotumika katika kuzuia matangazo ya tumbaku na kutoa elimu zaidi, hali itakuwa mbaya kwani ukuaji wa magonjwa yasioambukiza unachangiwa zaidi na tumbaku.

Mratibu Programu ya Usalama Barabarani kutoka Shirika la Afya Duniani, Merry Kessi amesema vifo milioni 7.2 kote duniani kila mwaka husababishwa na matumizi ya tumbaku.

“Kati ya vifo hivyo wanaoathirika ni wale wanaopokea moshi utokanao na tumbaku ambao ni wanawake na watoto wengi hufariki kwa saratani mbalimbali,” amesema Kessi.

Mtaalamu wa magonjwa ya saratani kutoka Hospitali ya Ocean Road, Dk Maghuha Stephano amesema kemikali inayotoka kwa mtu anayevuta huwa sumu mbaya zaidi ikipokewa na mtu mwingine.

“Ile kemikali iliyopo kwenye sigara mtu anapokuwa anavuta, ule moshi unaotoka nje ndiyo una sumu nyingi zaidi kuliko ule unaoingia kwa mvutaji,” amesema.

Pia Soma

Dk Maghuha amesema madhara ambayo yanaweza kumpata mtu anayepokea moshi wa sigara kutoka kwa mvutaji, anaweza kupata matatizo ya kawaida kwenye njia za hewa kama kupaliwa na hata magonjwa ya mfumo huo.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya saratani Ocean Road, Crispin Kahesa amesema kwa kawaida mtu huvuta hewa safi na ikifika ndani huchujwa na taka sumu hutoka, hivyo mvutaji anapouvuta moshi wa tumbaku ule utokao hutoka na sumu nyingi zaidi.

“Tumbaku ndiyo chanzo cha aina zote za saratani, japokuwa kuna zile ambazo athari ni kubwa zaidi kama saratani za mfumo wa hewa ikiwemo mapafu, njia ya chakula, lakini hata ikifika sehemu nyingine inaleta madhara,” amesema.

Zijue kemikali zenye madhara zilizo kwenye sigara

Wataalamu wanabainisha kuwa uvutaji sigara huathiri mwili kwa njia tofauti na madhara yake ni makubwa kiafya.

Inakadiriwa kuwa, hadi sasa kumegunduliwa kemikali zipatazo 7,000 katika moshi wa sigara ambapo 250 kati ya hizo ni sumu na 70 zinasababisha saratani.

Mvutaji mdogo hutumia nusu ya pakiti ya sigara kwa siku na kujikuta akiathiri mwili wake kwa kemikali hizi mara 3500 kwa mwaka.

Moshi na kemikali zilizo kwenye sigara huathiri karibu kila kiungo mwilini kuanzia seli hadi mfumo wa kulinda mwili.

Kemikali zilizoko kwenye moshi wa sigara huingia katika mapafu na kuenea katika mwili mzima na kusababisha madhara makubwa kwa njia mbalimbali.

Chanzo: mwananchi.co.tz