Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tsh.250 Milioni zajenga kituo cha afya Handeni

Hande 3 Moja ya majengo mapya

Wed, 9 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, Saitoti Stephen amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia halmashauri yake fedha zitokanazo na Makusanyo ya Tozo za miamala ya simu Shilingi Milioni 250 ambazo zimefanikisha kukamilisha ujenzi wa Kituo Cha Afya Cha Tarafa ya Sindeni.

"kwa kipindi Cha kuanzia 5 September mwaka Jana Tulifanikiwa Kupatiwa fedha na Rais Samia Suluhu Hassan mgao wa Milioni 250 kwaajil ya kuanza ujenzi wa Kituo Hiko na Hadi kufikia tarehe 31 December mwaka Jana kituo hicho Cha Afya kiliamilika" Amesema Mkurugenzi huyo.

Aidha, Amesema kwa Sasa halmashauri yake inaendelea kuhakikisha kituo Hiko Cha Afya kinaanza kutoa Huduma ya Afya mapema mwaka huu kwakuwa jengo la Wagonjwa wa nje,Maabara pamoja na sehemu ya kichomea Taka vyote vimeshakamilika kwa ubora uliokusudiwa.

"Wananchi wangu walikua wanatembea umbali wa zaidi ya kilometa 80 kufuata Huduma ya Afya lakini kukamilisha kwa kituo hiki Cha Afya kitawasaidia kutatua changamoto hiyo" Ameongeza mkurugenzi Saitot.

Hata hivyo ameendelea kusema kwamba halmashauri yake imejipanga kwaajili ya Usimamizi wa Miradi ya kimaendeleo.

Ikumbukwe kwamba Halmashauri ya WIlaya ya Handeni Ina Tarafa tano lakini katika Tarafa hizo ni Tarafa mbili pekee zilikua na vituo vya Afya ambavyo Ni kituo Cha Afya Cha Mkata pamoja na Kabuku,lakini kukamilisha kwa ujenzi wa kituo Cha Afya Cha Tarafa ya Sindeni uongeza idadi ya halmashauri Kuwa na vituo vya afya vitatu katika halmashauri hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live