Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tozo za Miamala zajenga vituo 200+ vya Afya Vijijini

Afyaaaa Tozo za Miamala za jenga vituo 200+ vya Afya vijijini

Wed, 1 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amesema kuwa Tozo za Miamala ya simu, zimesaidia katika kuboresha huduma za kijamii kwa kujenga vituo 220 vya afya ndani ya mwezi mmoja wa makusanyo hayo.

Waziri huyo amesisitiza kwa kusema kuwa, wakati Rais Samia anaingia madarakani takribani tarafa 217 zilikuwa hazina vituo vya afya, hivyo amewataka wananchi kufurahia tozo hizo kwani zinaleta maendeleo kwa wote.

“Wakati Rais anapokea kijiti kulikuwa na tarafa 217 hazina vituo vya afya, tukaweka malengo kwamba ukiweka na nyingine za kijiografia tukaenda target ya 220, makusanyo mpaka ya jana tunapeleka fedha nyingne kwa maana hiyo kwa Mwezi mmoja na nusu tumepata fedha za kujenga vituo 220 kwenye tarafa hizo ambazo zilikuwa hazina vituo vya afya tangu kupata uhuru sasa si mnaona hapo kwamba ni vema tu tuangalie viwango visituumize sana ila nia ya Rais ya kupeleka vituo vya afya kwenye tarafa zote ni nzuri”-- Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba.

Ameongeza kusema kuwa, vituo vyote hivyo vina uwezo wa kufanya upasuaji, na vitasaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto kwa upana.

Katikati ya hilo, Waziri Nchemba aliwainukia wale wanaolalamika juu ya Tozo hizo kwa kujiita maskini na kuwa tozo hizo zipo kuwadidimiza amewataka kuacha hoja hizo kwani malengo ya tozo ni kuwagusa maskini wa kweli wasio na vituo vya afya vijijini.

“Kuna Watu wanapenda kujiita masikini lakini hawa waliopo vijijini wale masikini ndio Mama anakwenda kuwagusa wale ambao anaweza kupoteza maisha kwasababu hakuna Hospitali karibu nae, aliyepo Mjini anaweza kuchagua aende Hospitali ipi iwe za Serikali au Binafsi, anaweza kwenda Muhimbili akafika pale akasema ngoja niende Regency”-- Alisisitiza Waziri huyo Wa Fedha.

Hata hivyo, alisema kuwa malengo na mikakati ya Rais Samia juu ya Tozo hizo sio tu kujenga miundombinu hiyo kwenye ngazi ya tarafa pekee, bali itafika katika ngazi ya kata pia, na kinachotazamwa zaidi kwa sasa ni kuboresha madarasa ili kuinua elimu ya watoto nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live