Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tohara si chanzo cha maumbile madogo kwa Mwanaume

Tohara Tohara Uume Tohara si chanzo cha maumbile madogo kwa Mwanaume

Tue, 17 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika baadhi ya Jamii huwa hawatahiri Wanaume kabisa, na wengine wanaotahiri husubiri hadi Mtoto afikishe walau Miaka 12 ndipo hutahiriwa kwa uoga wa kupunguza ukubwa wa Maumbile ya Kiume ya mtoto.

Hii ni nadharia tuu kwani ukuaji wa viungo vyote vinavyounda Mwili wa Binadamu huongozwa na Mifumo rasmi kuanzia kwenye Vinasaba (Genes) vya urithi pamoja Homoni mbalimbali za Mwili.

Tohara inaweza kufanyika muda wowote, kwa Watoto wachanga pamoja na Watu wazima. Hata hivyo tafiti zimeonesha uponaji wa haraka huonekana kwa Watoto kwa kuwa bado hawajafikia Umri wa kuonesha mwitikio wa hisia za Kimapenzi zinazosababisha Uume usimame mara kwa mara kwa Watu wazima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live