Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tohara kufikia asilimia 90 ya wanaume wasiotahiriwa Geita

F7a9fbaf4fe5aece4b14d86459a37a7c Tohara kufikia asilimia 90 ya wanaume wasiotahiriwa Geita

Sun, 1 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

AWAMU ya tatu ya kampeni ya tohara kwa wanaume nchini inayotekelezwa mwaka wa fedha 2021/2022 inatarajiwa kuwafi kia zaidi ya asilimia 90 ya wanaume ambao hawajafanyiwa tohara mkoani Geita ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi mkoani hapa.

Hayo yalisemwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa na Mratibu wa Huduma za Afya mkoani Geita, Vunza Mohamedi wakati wa kikao cha uraghabishi wa huduma ya tohara kilichojadili mpango wa huduma endelevu za tohara kwa wanaume inayoratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Tamisemi na ofisi ya mkuu wa mkoa.

Vunza alisema hamasa ya tohara kwa wanaume imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka, ambapo kwa mwaka 2019/2020 walikusudiwa kutahiriwa wanaume 52,890 kati yao, ni wanaume 42,026 walitahiriwa sawa na asilimia 79, huku kwa mwaka 2020/2021 walikusudiwa kutahiriwa ni wanaume 38,502, lakini wanaume 33,925 sawa na asilimia 88 walitahiriwa.

Katibu Tawala Mkoa wa Geita, Musa Chogelo aliwaomba wanaume ambao hawajafanyiwa tohara kuhudhuria kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili waweze kutahiriwa ili kuondokana na hatari za kupata maambukizi ya magonjwa yatokanayo na kujamiiana kama ukimwi kwa zaidi ya asilimia 60 kama tafiti zinavyoonesha.

Chogelo alisema takribani miaka 11 tangu kuanza kwa utekelezaji wa afua ya tohara kwa wanaume nchini, Tanzania imepata mafanikio makubwa katika utekelezaji kwani tafiti na matokeo ya VVU na ukimwi zinaonesha kiwango cha tohara kwa wanaume kimeongezeka kutoka asilimia 67 mwaka 2007 hadi asilimia 77.4 mwaka 2017.

Alisema kwa mujibu wa takwimu za Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi, hadi sasa zaidi ya wanaume milioni sita wametahiriwa kwenye mikoa ya kipaumbele ndani ya miaka 10, ambapo utekelezaji wa kampeni hiyo umesaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz