Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tibu ukavu wa nyayo zako

D47eeea116a58d4a58450229d6406a53 Tibu ukavu wa nyayo zako

Sun, 19 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WATU wengi hutamani kuwa na nyayo za miguu laini na nzuri zenye kuvutia kwenye macho ya watu, lakini inashindikana na kujikuta wakiwa na nyayo kavu zisizovutia kuonekana machoni mwa watu.

Kwa kawaida ngozi ya kwenye nyayo huwa ni kavu ukilinganisha na ngozi ya maeneo mengine mwilini lakini mwanamke au mwanamume mwenye kujali muonekano wake hadharau afya ya ngozi ya miguu yake.

Vitu vinavyosababisha ukavu mpaka kupasuka nyayo ni kutembea sana peku, ukali wa jua na miguu unaikanyaga chini. Tatizo la kisukari na taifodi, kuogea maji ya moto kupitiliza kila siku, matatizo ya ngozi ‘eczema’ ni vitu ambavyo husababisha ngozi kuwa kavu.

Kutibu ukavu wa nyayo Osha miguu yako kwa maji safi na sabuni kisha ikaushe, hakikisha unapaka nyayo zako mafuta au losheni, usipake losheni zenye kemikali au alcohol huzidisha ukavu wa miguu.

Paka hata mafuta ya watoto ambayo hayana kabisa kemikali au mafuta ya nazi au ya mzeituni. Unaweza kulowe- ka miguu yako kwenye maji ya uvugu uvugu uliyoyakamulia maji ya limao kwa dakika tano kusaidia kuondoa zile seli zilizokufa, kisha ioshe vizuri na upake mafuta ya vaseline.

Paka miguu yako mchangan- yiko wa kijiko kimoja cha mafuta ya mzeituni na matone kad- haa ya limao. Changanya vyema kisha paka kwenye nyayo ili kuipa unyevu unyevu.

Mafuta ya nazi Kabla ya kulala chukua mafuta ya vaseline ujazo wa kijiko kidogo cha chai na kamulia limao zima kisha koroga vyema huo mchanganyiko kisha paka kwenye nyayo zako, fanya hivi ukiwa umenawa miguu na umeifuta vizuri imekauka ndio unapaka. Vaa soksi zako ndio upande kitandani kulala.

Chanzo: habarileo.co.tz