Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tiba watoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi IFM

Fri, 7 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chama cha madalali wa bima Tanzania (TIBA), kupitia kampuni ya bima ya Metropolitan kimetoa ufadhili wa ada kwa wanafunzi watatu wa Chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM).

Wanafunzi hao wa mwaka wa tatu katika fani ya Shahada ya bima wamepokea msaada huo ikiwa  ni mwendelezo wa utekelezaji wa kipengele kilichomo ndani ya Mkataba wa Makubaliano kati ya TIBA na IFM kilichowataka kudhamini wanafunzi wenye mahitaji kila mwaka.

Akizungumza leo Septemba 6 wakati wa kutoa msaada huo, Mkurugenzi Mtendji wa Metropolitan, Suresh Kumar amesema msaada huo wa Sh4.5 milioni utasaidia kufanikisha ndoto za wanafunzi hao zilizokaribia kuzimika kutokana na changamoto.

"Hawa ni wanafunzi wa mwaka wa tatu ambao wanaelekea kumaliza masomo lakini walikuwa wakikutana na changamoto za kukosa ada na matumizi mengine jambo ambalo lingewayumbisha katika masomo yao na huenda wangeshindwa kumaliza," amesema Kumar na kuongeza:

"Wapo wengi wenye mahitaji lakini hatuwezi kuwasaidia wote kwa pamoja licha ya kuwa tunatambua kuwa hakuna urithi wala msaada bora wa kumpatia mtu kama maarifa."

Mmoja wa wanafunzi waliopokea msaada huo Rhoda Carol amesema ukosefu wa fedha za matumizi na ada ni kikwazo kwa wanafunzi wengi  wasio na uwezo na kuwaomba wafadhili mbalimbali kuwasaidia ili wamalize masomo.

"Tutajitahidi tuwe mfano mzuri ili wafadhili wetu waweze kujivunia na kuona hawajafanya makosa katika kutuchagua sisina wavutiwe kuwapa wengine fursa ya ufadhili,"amesema Rhoda.

Chanzo: mwananchi.co.tz