Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tiba saratani ya matiti bila kukatwa yaingia Tanzania

50109 SARATAN+PIC

Wed, 3 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wanawake wanaougua saratani ya matiti sasa wamepata ahueni baada ya njia mpya ya tiba ya ugonjwa huo kufanyika pasipo kukata kiungo hicho.

Awali matibabu ya saratani ya matiti yalitolewa nchini kwa njia ya kuondoa kabisa titi katika hatua yoyote ya ugonjwa.

Hatua hiyo imekuja baada ya Serikali kununua mashine ya tiba za saratani itakayokuwa na uwezo wa kupanga tiba inayomfaa mgonjwa (CT Simulator) na mbili za mionzi inayotumia teknolojia ya kisasa yaani ‘3D’ aina ya Linear Accelerators (LINAC).

Akizungumza na Mwananchi katika hospitali ya Mloganzila leo Aprili 2, 2019 daktari bingwa wa upasuaji wa matiti kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Gasper Haule amesema wanatarajia kufanya upasuaji kwa wagonjwa wanne wanaougua saratani hiyo mapema wiki hii.

“Tiba hii inafanywa kwa wale ambao wamegundulika kuwa saratani ipo katika hatua ya kwanza na ya pili, tutawafanyia upasuaji, tutatoa vivimbe na kisha watapewa tiba ya mionzi kwa kutumia mashine za kisasa zilizopo Ocean Road,” amesema.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili tawi la Mloganzila, Dk Julieth Magandi amesema njia hiyo mpya ya tiba ya saratani ya matiti imewakusanya wataalamu wa upasuaji wa matiti kutoka nchini Kenya, Ocean Road, Bugando, KCMC, Muhimbili na Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.



Chanzo: mwananchi.co.tz