Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Temeke, Kigamboni, Sumbawanga vinara wa uchafu Tanzania

28530 Choo+pic TanzaniaWeb

Sun, 25 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Wakati wilaya ya Njombe ikibeba makombe lukuki ya ushindi katika masuala ya vyoo na usafi, wilaya mbili za Jiji la Dar ea Salaam zimeshika mikia.

Akizungumza leo Ijumaa Novemba 23, 2018 jijini Dodoma, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema Serikali ilishindanisha halmashauri mbalimbali na majiji kwa vigezo vilivyowekwa.

Ameitaja wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa kuwa ya mwisho ikifuatiwa na wilaya za jiji la Dar es Salaam za Temeke na Kigamboni.

Katika kundi la manispaa na majiji, Iringa wamekuwa vinara wakifuatiwa na Arusha na Moshi ambao mwaka huu wameshika nafasi ya tatu.

Njombe ilishinda katika makundi yote ikiwemo hospitali, vijiji na shule na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amehoji kwa nini wengine wameshinda halafu maeneo mengine wameshindwa.

Majaliwa ameziagiza halmashauri na majiji kutoona aibu badala yake wakajifunze kwa Njombe.



Chanzo: mwananchi.co.tz