Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Teknolojia mpya kufuatilia maendeleo ya mtoto yatambulishwa

517e394d756ff16358abc456be068bfd Teknolojia mpya kufuatilia maendeleo ya mtoto yatambulishwa

Mon, 14 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAASISI isiyokuwa ya kiserikali ya Kamanga Health Care Foundation (KHF) imetambulisha rasmi matumizi ya teknolojia inayofahamika kama Non-Stress Test (NST) kwa wajawazito ili kufuatilia maendeleo ya mtoto tumboni.

Akizungumzia teknolojia hiyo mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Dk Mercy Minde alisema wataanza kuitumia teknolojia hiyo mwezi ujao na inalenga kusaidia serikali kutoa huduma za afya kwa gharama nafuu na kwa wakati, hasa kwa makundi maalumu.

Dk Minde alisema miongoni mwa makundi ambayo taasisi hiyo imeyalenga ni kundi la wanawake wajawazito na kuwa matumizi ya teknolojia ya NST itawasaidia kutambua mapigo ya moyo ya mtoto tumboni na hivyo kumpatia mama tahadhari na huduma kulingana na mabadiliko yatakayobainika ili kukabili changamoto zinazoweza kumfanya mama ama mtoto kupoteza maisha.

Dk Minde ambaye pia ni Daktari Bingwa wa watoto alisema mbali na huduma ya afya ya mama na mtoto pia taasisi hiyo imedhamiria kujikita katika kutoa mafunzo kwa wauguzi, kusaidia huduma za upasuaji, huduma za kinywa na meno na huduma za uchunguzi na tiba kwa gharama nafuu.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando, Dk Fabian Masaga aliipongeza taasisi hiyo kwa kuja na matumizi ya NST kwani afya ya mama na mtoto ni eneo nyeti na kuwaomba watoa huduma za afya wote kutoka taasisi binafsi na zile za serikali kuwajibika kikamirifu kuisaidia serikali kufikia adhima ya kumaliza vifo vya watoto wachanga.

Chanzo: habarileo.co.tz