Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tasisi kutoa elimu ya dawa za kulevya shule za sekondari

16175 Pic+dunia TanzaniaWeb

Sun, 9 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Taasisi ya kusaidia Vijana wanaotumia dawa za kulevya ya Dunia Moja Pamoja imejipanga kutoa elimu katika shule za sekondari nchi nzima ili kuhamasisha vijana wasiingie kwenye mkumbo wa uvutaji wa dawa hizo.

Akizungumza leo Septemba 7, 2018 wakati wa uzinduzi wa kampeni za utoaji wa elimu hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Saida Kessy amesema wanatoa elimu hiyo ili vijana wajiepushe na makundi au mazingira yanayoweza kuwaingiza kwenye uvutaji wa dawa za kulevya.

“Ni vyema kijana akapata elimu ili asiingie kwenye matumizi ya dawa za kulevya, kuliko aanze kutumia ndipo apate elimu. Kinga ni bora kuliko tiba,” amesema.

"Hii taasisi yetu ilianzia mkoani Arusha na tumeshatoa elimu katika shule zaidi ya 20 za sekondari hivyo leo hii tumekuja hapa Dar es Salaam kwa ajili ya kuizindua lengo letu sasa kuzunguuka nchi nzima kutoa elimu kwenye shule hizo,"ameongeza

Amesema wamefanya tathmnini wamebaini kuwa vijana wengi wanaoingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya hawafahamu athari zake hivyo elimu hiyo itawapa mwanga wa athari za dawa hizo.

Mhamasishaji wa taasisi hiyo ambaye ni muathirika wa dawa za kulevya, Jonas Kessy amesema hakuna umuhimu wa kumtupa jela mtumiaji wa dawa za kulevya kwani huenda akaathirika zaidi au akitoka akaendelea kutumia.

"Mfano unapoingizwa jela utatumikia kifungo lakini ukitoka utaendelea kuvuta dawa za kulevya kama angepewa elimu angeweza kujitambua siyo kumlazimisha kuacha kwa kumpeleka jela,"amesema Kessy.

Chanzo: mwananchi.co.tz