Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yavunja rekodi matibabu ya moyo

Moyo Mloganzila.jpeg Tanzania yavunja rekodi matibabu ya moyo

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Upasuaji mdogo wa moyo wa kubadilisha valvu ya mshipa mkubwa wa damu bila kufungua kifua umefanyika kwa wagonjwa watatu wenye umri wa zaidi ya miaka 70 katika kambi maalumu ya matibabu ya siku mbili iliyofanywa na wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Hospitali ya Starcare ya nchini India.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. John Jingu amesema uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika sekta ya afya ikiwa ni pamoja na kujenga majengo ya kisasa, kusomesha wataalamu na kununua vifaa tiba vya kisasa kumewezesha kufanyika kwa upasuaji huo.

Kwa Julai hadi Disemba mwaka huu alidokeza kuwa JKCI imehudumia zaidi ya wagonjwa 3,000 katika kufanya upasuaji mkubwa na mdogo wa moyo na kusisitiza Serikali itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kibingwa za matibabu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter Kisenge almeishukuru Serikali kwa kuiwezesha taasisi hiyo ambayo imeweza kufanya matibabu hayo ya kihistoria ambapo kwa nchi za Afrika hakuna hospitali ya Serikali inayotoa huduma hiyo.

Aidha, amesema JKCI imeendelea kuwa kituo cha utalii tiba ambapo wagonjwa kutoka nchi 20 za Afrika zinafika kwenye taasisi hiyo kupata matibabu kutokana na wingi wa wagonjwa, aliiomba Serikali jengo lingine kwaajili ya kuwahamishia wagonjwa ombi ambalo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Jingu alisema linafanyiwa kazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live