Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yatuma madaktari bingwa 12 kwenda Zambia

Madaktari Tanzania yatuma madaktari bingwa 12 kwenda Zambia

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Tanzania imetuma madaktari bingwa 12 kwenda nchini Zambia kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo kwa watoto hii ikiwa ni sehemu ya kuendelea kutanua wigo wa tiba utalii na kukuza mahusiano baina ya nchi hizi mbili.

Wataalamu hao kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete(JKCI) ambao watakaa nchini humo kwa wiki mbili wanatarajiwa kutoa matibabu ya upasuaji mkubwa wa magonjwa ya moyo hususani kwa watoto chini ya miaka 15 na kuisaidia nchi ya Zambia kuanzisha huduma ya matibabu ya moyo nchini humo.

Hayo yamebainishwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel wakati akizungumza na vyombo vya habari juu ya huduma za mkoba (outreach services) za matibabu ya kibingwa nje ya Tanzania kutoka JKCI.

Dk. Mollel amesema kuwa katika uwekezaji mkubwa aliofanyika katika sekta ya afya na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika teknolojia, kusomesha wataalamu, miundombinu ya hospitali imeleta mapinduzi makubwa mpaka Tanzania kuwa kitovu cha tiba utalii Afrika Mashariki.

“Lengo la Tanzania kuwa na madaktari bingwa na miundombinu ya kutoa Huduma za kibingwa na bingwa bobezi ni kuhakikisha fedha ya kigeni haiendi nje ya nchi ili kusaidia kugharamia watanzania wasaio kuwa na uwezo wa kupata matibabu hapa nchini”, ameeleza Dk. Mollel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live