Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yatajwa kuongoza kwa TB

30459 TB+PIC Mkurugenzi wa huduma za tiba kutoka Wizara ya Afya, Dk Leonard Subi

Thu, 6 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Tanzania imetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi 30 duniani zenye maambukizi makubwa ya ugonjwa wa kifua kikuu (TB), huku ugunduzi wa wagonjwa hayo ukiwa chini.

Kati ya wagonjwa wote wanaougua TB nchini, ni asilimia 44 waliogundulika na kuanzishiwa dawa. Hayo yalielezwa jana jijini Dodoma na mkurugenzi wa huduma za tiba kutoka Wizara ya Afya, Dk Leonard Subi akizungumza na wataalamu wa afya na waratibu wa kifua kikuu kutoka mikoa na halmashauri zote nchini.

“Kati ya Watanzania 100,000, 266 wameambukizwa TB, hii haichagui mwanamke, mwanaume, kijana wala wazee,” alisema.

Naye meneja wa kudhibiti ugonjwa huo na ukoma wa Wizara wa Afya, Dk Beatrice Mtayobwa alisema lengo ni kupunguza maambukizi ya TB kwa asilimia 30 kufikia mwaka 2020.



Chanzo: mwananchi.co.tz