Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yashindwa kufikia adhima ya upimaji afya za wananchi

Mon, 3 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Tanzania ililenga kupima watu zaidi ya milioni 4.6 ili kutambua afya zao lakini waliopima hadi Novemba, 2018 walikuwa ni 2.4 milioni.

Takwimu hizo zimetolewa leo Jumamosi Desemba 1, 2018 na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, DK Faustin  Ndungulile ambaye amesisitiza kuwa dawa ya Ukimwi haijapatikana bado.

Dk Ndungulile amesema kati ya waliopima,  wanaume walikuwa ni asilimia 44 lakini akasema hadi sasa zaidi ya Watanzania 1.5 milioni wamebainika kuwa na VVU.

Awali, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dk Leonard Maboko amesema watu 262,114 wamepima afya zao katika kampeni ya furaha yangu ikiyozinduliwa na Waziri Mkuu Juni 19, 2018

Kati ya idadi hiyo, wanaume ni 125725 sawa na asilimia 48 ni wanaume huku wanawake wakiwa ni 136389 ambao ni asilimia 52 hiyo ni kwa kampeni ya furaha yangu pekee.

Dk  Maboko ametoa taarifa hiyo leo Desemba Mosi,  2018 kwenye taarifa yake kwa Waziri mkuu katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI  dunia.

Mkurugenzi ameutaja mkoa wa Mwanza kuwa uliongoza katika kampeni hiyo kwa kupima watu 132226 ukifuatiwa na mkoa wa Tabora 55858 na Njombe walipima watu 24125.



Chanzo: mwananchi.co.tz