Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yalegeza masharti ya Uviko 19

Ummy Mwalimu Uviko.jpeg Waziri wa Afya Ummy Mwalimu

Wed, 16 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo March 16, 2022 Tanzania inatimiza miaka miwili kamili tangu kuthibitika kwa uwepo wa Ugonjwa wa virusi vya corona (UVIKO-19) kwa mara ya kwanza nchini, akitoa tamko la hali ya ugonjwa huo kwa miaka miwili tangu kuripotiwa kwake Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Kwa kuzingatia hali ya sasa ya maambukizi ya UVIKO-19 nchini na mwenendo wa ugonjwa huu duniani, Serikali inalegeza masharti kwa Wasafiri wanaoingia nchini ambao wamekamilisha dozi ya chanjo ya UVIKO-19 kuanzia kesho.

"Miaka miwili ya mapambano dhidi ya UVIKO 19 nchini Tanzania UVIKO 19 bado upo nchini na duniani, chanjo ndio njia kuu kwa sasa katika kujikinga na kukabiliana na ugonjwa huu, nawahimiza Wananchi Kuchanja"

"Pili, tumelegeza masharti kwa wasafiri wanaoingia nchini na ambao wamechanja chanjo ya UVIKO19, kuanzia kesho tar 17 Machi 2022 hakuna Negative RT - PCR Certificate before arrival in Tanzania, karibuni Tanzania"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live