Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yakanusha uwepo wa kirusi kipya cha Uviko 19

Kirusipic Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza

Wed, 23 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati kirusi kipya cha Uviko 19 kikibisha hodi katika mataifa kadhaa yakiwemo ya Afrika, kirusi hicho bado hakijafika Tanzania.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati akipokea chanjo aina ya Sinovac kutoka serikali ya Uturuki.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati akipokea chanjo aina ya Sinovac kutoka serikali ya Uturuki.

Amesema taarifa alizopata hadi leo asubuhi ni kwamba kirusi kilichopo nchini ni Omicron pekee na hiyo ni kwa mujibu wa uchunguzi wa kitaalam wa sampuli.

Amesema mataifa mengine yameshaanza kupata kirusi kinachotokana na muunganiko wa Delta na Omicron.

“Asubuhi nilikuwa naonge na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu hicho kirusi kipya wakaniambia bado wanaendelea kufanya tafiti kujua kitakuwa kikali kiasi gani na madhara yake yatakuwaje.

“Habari njema ni kwamba na sampuli nilizoelekeza zichukuliwe kuangalia kama tuna kirusi hicho zimeoonyesha hatuna bado tuna Omicron,” amesema Ummy.

Advertisement Kufuatia hali hiyo amesisitiza watu kupata chanjo ya Uviko itakayosaidia kukabiliana na ugonjwa huo.





Chanzo: www.tanzaniaweb.live