Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yakabiliwa na upungufu wa madaktari wa macho

21287 Macho+pic TanzaniaWeb

Mon, 8 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Tanzania ina madaktari bingwa wa macho 55 ambao wanatoa huduma kwa watu zaidi ya milioni 50.

Hiyo ni sawa na wastani wa daktari mmoja kwa watu milioni moja, kiwango ambacho ni kikubwa ukilinganisha na wastani wa dunia unaotaka daktari mmoja kuhudumia watu 400,000.

Kaimu Rais wa Madaktari wa Macho nchini, Dk Cyprian Gabriel amesema idadi ya madaktari hao pia ni wale walioko mijini lakini wanakabiliwa na upungufu wa vifaa tiba wakati vijijini hawana kabisa huduma hizo.

Gabriel ametoa kauli hiyo wakati akitoa taarifa ya ugonjwa wa macho leo Oktoba 7, 2018 jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya siku ya macho duniani.

"Mheshimiwa mgeni rasmi, tatizo ni kubwa kuliko watu wanavyofikiria, madaktari ni wachache sana wakati tatizo ni kubwa zaidi vijijini," amesema Dk Gabriel

Mganga huyo amesema tatizo la watu wengi kujiita ni madaktari bingwa wa macho wakati ni vishoka na wamekuwa wakisababisha usugu wa magonjwa kwani wanapotibia watu huwa wanawaumiza zaidi.

Kaimu mganga mkuu wa Serikali, Dk Eliud Eliakimu amesema tatizo la macho ni kubwa duniani kote kwani takwimu zinaonyesha watu 255 milioni wanaugua macho duniani.

Dk Eliakimu ametangaza vishoka wanaotibu macho kusakwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwani wanakuwa chanzo cha upofu kwa watu hata pale ambapo wangeweza kutibika.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz