Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yaanza udhibiti Ebola mipakani

Ebola Case23 Tanzania yaanza udhibiti Ebola mipakani

Wed, 21 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Tanzania imeanza kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji katika mipaka ya nchi na viwanja vya ndege kupitia mikakati sita ili kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Ebola uliotangazwa nchini Uganda usiingie nchini.

Jana Uganda ilitangaza mlipuko huo baada ya watu sita kufariki huku mgonjwa mmoja vipimo vya maabara kuthibitisha kuwa anaugua ugonjwa huo katika Wilaya ya Mubende iliyopo katikati ya nchi hiyo.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Septemba 21, 2022 Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Aifelo Sichwale amesema wamepitia tahadhari zote na kuamsha utayari na mifumo na ule wa majibu kwa kuangalia utayari wake wa kufanya kazi.

Amesema tayari wameandaa taratibu za mwelekeo wa timu za dharura au RRTs ngazi zote kuanzia Taifa hadi Halmashauri.

“Waganga wakuu wa mikoa Tanzania Bara wamejulishwa mikoa yote na ile yenye riski kubwa imebainishwa na wote wanaendelea na maandalizi. Mikoa hiyo ni Kagera, Mwanza, Geita, Mara, Kigoma, Arusha, Dar es salaam na Kilimanjaro,” amesema.

Dk Sichwale amesema timu za afya mipakani zimejulishwa kuwa katika hali za uendeshaji mipaka yote, kipaumbele ikiwa mipaka na viwanja vya ndege vya kimataifa vilivyopo katika mikoa tajwa.

Amesema tayari wamerejesha upimaji wa kuchunguza kupitia thermoscanner katika mipaka hiyo na viwanja vya ndege vya Kilimanjaro (KIA) na viwanja vyote vya Mwalimu Nyerere vilivyopo Dar es Salaam (JNIA).

“Tumeandaa timu za ufuatiliaji ikiwemo anuani za wasafiri na wanakotokea, timu za kuondoa uchafuzi, timu za matibabu, mavazi maalum ya kujikinga kwa watoa huduma wa afya PPEs zinapitiwa na kusambazwa kuona namna tunaweza kudhibiti ugonjwa huo.

“Tamko litatolewa leo na Waziri wa Afya kuelezea hatua za wananchi kuchukua ili kujikinga na ugonjwa huu,” amesema Dk Sichwale.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live