Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania ni miongoni mwa nchi inayoathirika zaidi na seli mundu

Wed, 19 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

T: Tanzania ni miongoni mwa nchi inayoathirika zaidi na seli mundu

 

S: Tanzania imeungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku ya seli mundu duniani ambayo huadhimishwa Juni 19 kila mwaka.

 

Asna Kaniki, Mwananchi

[email protected]

Pia Soma

Dar ea Salaam. Tanzania imetajwa kuwa nchi inayoathirika zaidi na ugonjwa wa Seli mundu ikilinganishwa na nchi nyingine duniani.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Juni 19 2019 na Daktari bingwa wa magonjwa ya damu kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (Muhas) Flora Ndobho katika maadhimisho ya siku ya seli mundu duniani inayoadhimishwa Juni 19 kila mwaka.

Amesema kila mwaka watoto 15,000 wanazaliwa na ugonjwa wa seli mundu huku asilimia 6 ya watoto hufa na ugonjwa huo kwa mwaka.

"Ugonjwa wa sickle cell (Seli mundu) ni miongoni mwa ugonjwa unaosumbua watu wengi, katika jamii na kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO)  zaidi ya asilimia 70 ya waathirika wa ugonjwa huu wako barani Afrika," amesema Dk Flora.

"Kwa hiyo leo tumeungana na wenzetu duniani kwa kuadhimisha siku hii kwa kukaa na wadau mbalimbali ya afya ili kujadili changamoto mbalimbali za ugonjwa huu ikiwemo matibabu.”

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dk Yudas Ndungile kutokana na uelewa mdogo wa wananchi juu ya seli mundu mkoa utaangalia namna ya kuanzisha kliniki za wataalamu wa ugonjwa huo ili kuweza kuwafikia wagonjwa katika maeneo mbalimbali.

Chanzo: mwananchi.co.tz