Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania ina zaidi ya watoto 35,000 wanaioshi mitaani

4c857a7d0b0d7ae78dee70c2c84efe65.jpeg Tanzania ina zaidi ya watoto 35,000 wanaioshi mitaani

Tue, 14 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema zaidi ya asilimia 90 ya watoto wanaoishi mitaani, wazazi au walezi wao wanafahamika. Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk John Jingu amesema jana jijini Dodoma kuwa, watoto wanaoishi na kufanya kazi au kuomba mitaani wapo hatarini kutumikishwa katika magenge ya kihalifu.

Amesema hayo wakati akifungua kikao kazi cha kuweka mikakati ya kumaliza changamoto ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani. Dr. John Amefungua mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo, Dk Dorothy Gwajima. Kikao hicho kilihudhuriwa na makatibu tawala wa mikoa, makamanda wa polisi wa mikoa, wakuu wa dawati la jinsia na watoto la Jeshi la Polisi na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhini (Latra).

Dk Jingu amesema tatizo hilo linasikitisha na halikubaliki, hivyo lazima lifanyiwe kazi pamoja na kufahamu chanzo cha watoto hao kuishi mitaani.

“Kundi hili la watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani liko katika hatari ya kutumikishwa katika magenge yasiyofaa ya kihalifu hivyo ni vyema tukawaangalia watoto hawa kwa jicho pana na la kipekee kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kuwaokoa kwa faida yao wenyewe, familia zao na taifa zima kwa ujumla,” alisema na kuongeza: “Utafiti uliofanywa mwaka 2017 katika mikoa ya Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya, Iringa na Dar es Salaam ulibaini jumla ya watoto 6,393 walikuwa wanaishi na kufanya kazi mtaani.” ________Dr. John

Amesema takwimu zinaonesha kuna watoto 35,919 wanaoishi na kufanya kazi mitaani katika majiji na miji nchini.

“Kwa msingi huu tumeona ni vyema kuwa na kikao hiki chenye wadau hawa muhimu ili tuweze kujadili na kuwa na mkakati wa pamoja unaolenga kuondoa changamoto hii,” _____Dr. John

Amesema watoto wengi badala ya kwenda shule wamekuwa wakikaa nyumbani na kujilea na wengine wakilelewa na watu wenye mienendo isiyokubalika kwenye jamii.

“Tatizo hili likiendelea tunatengeneza tatizo la kijamii kwa kutokuwa na watu wenye maadili, mfano jijini Dar es Salaam wanasema wanakaa na mabraza ambao ni wahalifu wakubwa,” alisema.

Ameongeza kuwa ingawa suala la watoto wa mitaani si la Muungano, jambo hilo linahitaji ushirikiano kwani linahusu mustakabali wa nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live