Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania ina vituo 600 vya kupima saratani za mlango wa kizazi, matiti

10311 Saratani+pic TZW

Fri, 29 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), Julius Mwaiselage amesema kuna vituo 600 vinavyoweza kupima na kubaini saratani za mlango wa kizazi na matiti.

Amesema changamoto iliyopo ni kuwa, havitoshi kwa sababu mahitaji ni makubwa.

Dk Mwaiselage akizungumza katika mjadala wa Jukwaa la Fikra uliandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL) Juni 28, 2018 amesema hata hivyo wahisani wanaendelea kusaidia.

Changamoto nyingine amesema ni kukosekana kwa huduma za uchunguzi wa tezi dume kwa baadhi ya maeneo au kama ipo kuna ukosefu wa vipimo vya ziada.

"Serikali imeendelea kuboresha eneo hilo ndiyo maana kuna vituo maalumu vya kutoa huduma hizo,” amesema.

Kuhusu tiba, amesema ni ya upasuaji, hivyo inatakiwa kuwawezesha wataalamu wengi zaidi ili kutoa huduma hiyo.

Dk Mwaiselage amesema pia kuna changamoto ya dawa ambazo zipo lakini huenda mgawanyo hauko sawa kwa maeneo ya mijini na vijijini.

Soma zaidi:

Profesa Swai atoa mbinu kuepuka kisukari

Waziri Mwalimu aipongeza MCL kuandaa Jukwaa la Fikra

Mapendekezo mjadala Jukwaa la Fikra kupelekwa serikalini

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz