Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, UNAIDS kukabiliana na Ukimwi

Ummy 1140x640.jpeg Tanzania, UNAIDS kukabiliana na Ukimwi

Sun, 29 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Tanzania na Shirika la UNAIDS zimekubaliana kuendeleza mashirikiano katika kukabiliana na UKIMWI.

Hayo yamebainishwa katika kikao pembezoni cha 75 cha Shirika la Afya Duniani kati ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na Winnie Byanyima, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishugulisha na masuala ya UKIMWI (UNAIDS).

Waziri Ummy amesema kuwa Tanzania inajivunia ushirikiano imara na wa kimkakati wenye manufaa na msaada kutoka kwa UNAIDS katika nyanja za uongozi, uundaji wa sera, na ukusanyaji wa rasilimali kwa ajili ya mwitikio wa kitaifa wa mapambano dhidi ya VIrusi vya UKIMWI.

Aidha ameeleza vipaumbele vya Tanzania katika mapambano dhidi ya UKIMWI ni pamoja na kupunguza maambukizi ya Virusi vya ugonjwa huo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto pamoja na kuzuia maambukizi vya UKIMWI kwa vijana na vijana balehe hususani vijana wa kike.

Naye, Byanyima ameupongeza utawala bora wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kuahidi utayari wa Tanzania kuunga Mkono azimio la kisiasa lililotangazwa na kutimiza malengo yaliyokubaliwa kwa miaka mitano ijayo katika kupambana ya UKIMWI.

Aidha, Bi Byanyima amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kuwa kinara wa uhamasishaji wa uchangiaji wa mzunguko wa saba wa Mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund).

Bi. Byanyima ameahidi kushirikiana na Tanzania katika kuhamasisha wafadhili wa kimataifa katika kutafuta rasilimali ambazo zitaleta matokeo makubwa katika kukabiliana na UKIMWI.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live