Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, Israel kushirikiana magonjwa ya moyo kwa watoto

Pediatric Cardiac Tanzania, Israel kushirikiana magonjwa ya moyo kwa watoto

Wed, 30 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania na Israel zimekubaliana kushirikiana kuboresha huduma za magonjwa ya moyo kwa watoto.

Makubaliano hayo ni kupitia Shirika la SACH linalojishughulisha na huduma za magonjwa hayo kwa watoto, ambapo tangu lianze kazi zake nchini mwaka 2015, limetoa matibabu kwa watoto 130.

Akizungumza wakati wa kikao hicho leo jijini Dodoma kati ya Wizara ya Afya na Simon Fisher, ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Shirika la huduma za Magonjwa ya Moyo kwa Watoto (SACH), Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi, amesema wamekubaliana kuendeleza ushirikiano katika masuala yanayohusiana na huduma hizo hapa nchini.

“Tumejadili kuongeza idadi ya wataalam watakaopata mafunzo ya muda mfupi na ya muda mrefu nchini Israel katika ubingwa na ubingwa bobezi wa magonjwa ya moyo kwa watoto,” amesema.

Alisema kupitia huduma hizo, Serikali imeweza kuokoa kiasi kikubwa cha fedha, kutokana na kupunguza idadi ya wagonjwa waliokuwa wakipewa rufaa ya kutibiwa nje ya nchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live