Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, China kushirikiana matibabu ya moyo

Moyo Dalili Shida Tanzania, China kushirikiana matibabu ya moyo

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

NCHI za Tanzania na China zimekubaliana kuanzisha mfumo wa wa pamoja wa upatikanaji wa vifaa tiba.

Vifaa hivyo vinavyotumika kutoa huduma za matibabu ya moyo kutoka nchini China ni muendelezo wa ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo na kutarajiwa kurahisisha upatikanaji wa vifaa vinavyotumika kutoa huduma za matibabu ya moyo na matibabu mengine yanayohitaji vifaa tiba.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Naibu Waziri Mkuu kutoka Serikali ya watu wa China Liu Guozhong.

Akizungumza Naibu Waziri wa Afya Dk Godwin Mollel amesema katika majadiliano imekubali kutoa msaada wa vifaa tiba nchini pamoja na kuanza kwa ushirikiano wa kuagiza vifaa tiba nchini China.

“Tumekubaliana kupitia Bohari ya Dawa (MSD) tutaenda kushirikiana na Serikali ya Watu wa China kupata vifaa tiba ambavyo mara nyingi tumekuwa tukiviagiza katika mataifa ya mbali na kuchukua muda mrefu kutufikia”, amesema Mollel

Amesema, Tanzania imejipanga kuhakikisha kuwa Bohari ya Dawa (MSD) inaenda moja kwa moja katika viwanda vilivyopo nchini China kununua vifaa tiba hivyo kupunguza gharama za matibabu.

“Tanzania tayari tuna sayansi kubwa, lakini vifaa mbalimbali vinavyotumika kila siku katika kutoa huduma za matibabu havipatikani hapa nchini kwasababu hatuna viwanda vinavyozalisha vifaa hivyo,”amesema na kuongeza.

“Haya ni matunda ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan, kwani tunapomuona akitembelea nchi mbalimbali duniani anafanya mambo makubwa ya ushirikiano na mataifa anayoyatembelea yaliyokuwa kisayansi na kiteknolojia ili kwa pamoja tujifunze na kutumia fursa zilizopo kuendeleza sekta yetu ya afya”,amesisitiza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dk Peter Kisenge amesema JKCI imekuwa moja ya Taasisi kubwa zinazotoa huduma za matibabu ya mogonjwa ya moyo barani Afrika, na kuwa yakwanza kufanya upasuaji mkubwa wa moyo na upasuaji wa moyo kwa watoto nchini yote hayo yakiwa ni matunda ya ushirikiano wa nchi ya Tanzania na China. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live