Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanga kujenga kituo cha mifupa

Malima.jpeg Mkuu wa Mkoa wa Tanga akifanya ukaguzi

Sun, 27 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima amesema mkoa wake unakusudia kuanzisha kituo cha Mifupa (Orthopaedic Centre) kwa ajili ya watu wanaopata ajali katika Barabara ya Mkata-Handeni na wakazi wa Tanga kwa ujumla.

Malima amesema hayo wilayani Handeni alipokuwa akikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya hiyo jana.

"Hii ndiyo njia kubwa baada ya hapa watu wanaopata ajali Dar es Salaam kituo cha kwanza labda ukatibiwe Tumbi (Kibaha mkoani Pwani), lakini ukishavuka Chalinze pale hakuna kituo kingine hadi unafika Tanga zaidi ya KCMC.

"Kwa hiyo tunataka hapa katikati tuwe na kituo cha kusaidia wanaopata ajali ambayo ni dharura. Kwa hiyo tumekubaliana, tumejenga hoja Wizara ya Afya imetusikia, Tamisemi (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) imetusikia kwa hiyo tujenge kituo pekee kitakachokuwa baina ya Tumbi na KCMC.

"Lakini wakati tunazungumzia kituo hicho hili jengo lilitakiwa liwe limekwisha sasa tutakuwa tunafanya kama ulafi fulani maana unakuwa kama unaomba chakula kingine wakati ulichokuwa nacho hakijaisha huo ni ulafi," amesema.

Malima amesema kukamilika kwa hospitali hiyo kutaamua hatima ya kituo hicho cha mifupa kwani nia ya kuwa nacho ni kubwa kutokana na umuhimu wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live