Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tamwa yataka mashirikiano na mitandao kupinga udhalilishaji

A7dacb7633069595f32b7140e19edcd0 Tamwa yataka mashirikiano na mitandao kupinga udhalilishaji

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Imelezwa kuwa mashirikiano ya pamoja kati ya Chama cha Waandishi wa habari Wanawake (TAMWA-Z’bar) na wanamitandao ya kupinga udhalilishaji inaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kumaliza ama kupunguza matendo ya udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto visiwani hapa.

Hayo yamelezwa na Afisa utafiti na tathmini kutoka TAMWA-Zanzibar, Mohamed Khatib wakati alipofungua mkutano wa siku moja wenye lengo la kuandaa mpango mkakati wa kupiga udhalilishaji mkutano uliofanyika katika ofisi za TAMWA-Tunguu Wilaya ya kati Unguja.

Alisema kupitia wanamitandao hao ambao watafanya kazi katika maeneo mbalimbali kutoka Wilaya tatu za Unguja ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano ya kijamii ambayo itawashirikikisha wananachi mbali mbali kupitia uongozi wa shehia na madawati ya kijinsia.

Pamoja na hayo alisema wapo baadhi ya watu wamekua wakikabiliwa na matukio ya udhalilishaji lakini huamua kukaa kimya kwa kutoona umuhimu wa kutoa taarifa hizo katika sehemu husika jambo ambalo hupelekea kuendelea kufanyika kwa matendo hayo.

Aidha alisema kwa kuliona hilo TAMWA-Z’bar kupitia maafisa hao watafanya kazi mbali mbali ikiwemo kutoa elimu kuhusu umuhimu wa wanajamii kutoa taarifa pamoja na kutambua viashiria vya udhalilishaji.

Akizungumza na kwa niaba ya washiriki wa mtandao kutoa kaskazini Unguja Hafidh Moh’d Juma alisema wamepokea jukumu hilo na kuahidi kulifanyia kazi kwa ufanisi mkubwa.

Alieleza kuwa miongoni mwa mada watazoziwasilisha na pamoja na umuhimu wa haki ya mtoto kwenye jamii kwa kuwa anaamini wapo baadhi ya watu wanashidwa kutambua haki za mtoto na ndio maana pengine wamekua wakifanyiwa matendo hayo.

Alisema watajikita pia kuzungumzia sheria ya ushahidi na umuhimu wa kutoa ushahidi kwa wanajamii katika keshi za udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto.

Nae Mwakilishi kutoka Wilaya ya magharib B Unguja Sharifa Hussein Said alisema watajikita kueleza viashiria ya udhalilishaji katika jamii.

Alieleza kuwa ipo haja kubwa kwa wanajamii hususani wazazi na walezi kufahamishwa namna bora ya kuvitambua viashiria vya udhalilishaji ili waweze kukabiliaana navyo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz