Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tamwa wazungumzia unyanyasaji wa wanawake katika vyombo vya habari

13337 Tamwa+pic TanzaniaWeb

Thu, 23 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi wa  Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa),  Eda Sanga amesema waandishi wengi wa kike wanakumbana na unyanyasaji wa kijinsia katika vyumba vya habari lakini wanaogopa kusema.

Akizungumza leo Jumatano  Agosti 22, 2018  katika mkutano wa masuala ya Jinsia na Habari ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), Eda amesema jambo hilo linaua taaluma ya waandishi wengi wa kike na kusababisha wakimbie taaluma hiyo.

Amesema hata utoaji wa kazi ndani ya vyumba vya habari nao umegubikwa na ubaguzi wa kijinsia.

“Utagundua kuwa waandishi wa kike wanapewa kazi za kuripoti habari nyepesi kama ni vipindi basi vya watoto au kilimo na sio masuala ya siasa na elimu," amesema.

Akizungumzia hilo Mkurugenzi wa kitengo cha Wanawake cha UN, Dk Phumzile  Mlambo- Ngucka amesema ni muhimu kumuinua mwanamke katika sekta zote.

Amesema kuna tatizo kubwa si tu katika vyombo vya habari bali hata katika ajira  na kipato.

"Lengo namba 5 la UN ni pamoja na kuweka uwiano wa kipato kati ya mwanamke na mwanaume. Wanawake wanalipwa kidogo ukilinganisha na wanaume,"amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz