Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tamwa: Bila usawa wa kijinsia, maendeleo ni ndoto

13295 Pic+tamwa TanzaniaWeb

Thu, 23 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wadau wa masuala ya jinsia nchini wamevitaka vyombo vya habari kuzingatia usawa wa kijinsia ili kufikia maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2025.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Agosti 22, wakati wa uzinduzi wa Mkutano wa jinsia na habari (Gender & News Summit) mkurugenzi wa Tamwa, Eda Sanga amesema bila usawa wa kijinsia ni vigumu kufikia maendeleo endelevu.

Amesema ni vyema kumuweka mwanamke mbele lakini pia bila usawa na haki kwa wanawake ni vigumu kwa jamii yoyote kupata maendeleo.

“Vyombo vya habari vinapoweka juhudi kubwa ambazo pia zinatoa nafasi kwa habari za kawaida za mama wa Kitanzania katika maisha yake kijamii, kifamilia, inakwenda kufanikisha malengo ya agenda yetu ya 2025 kama nchi lakini agenda ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa yatakuwa na mafanikio makubwa na kufikia katika hatua tunayoitarajia,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz