Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tamko la Chama Cha Madaktari kuhusu mgonjwa aliyefumuliwa kidonda

Nyuzi Ed Tamko la Chama Cha Madaktari kuhusu mgonjwa aliyefumuliwa kidonda

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: ippmedia.com

CHAMA cha Madaktari Tanzania (MAT) kimelaani vikali kitendo kilichofanywa na daktari wa Kituo cha Afya Kerege wilayani Korogwe mkoani Tanga, Jackson Meli, kufumua nyuzi kwenye jeraha la mgonjwa, kikisema ni kinyume na maadili ya taaluma ya kitabibu kimesema maadili ya taaluma yanaagiza daktari kutokuwa sehemu ya kusababisha madhara kwa mgonjwa kwa namna yoyote ile.

Tamko lililotolewa jana na Rais wa chama hicho, Dk. Shadrack Mwaibambe, lilieleza kuwa hatua za kisheria zifanyike ikiwamo kumfikisha mtuhumiwa wa tukio hilo katika baraza la kitaaluma.

"Tunapongeza mamlaka husika kwa kuchukua hatua stahiki za awali kwa mtuhumiwa na tunaomba utaratibu wa kisheria uchukue mkondo wake ikiwa pamoja na kufikishwa kwenye baraza Ia kitaaluma.

"Wanataaluma na hospitali zote zinakumbushwa kufuata utaratibu wa EMTALA 1986 ambao Tanzania imeridhia na inautekeleza. Mgonjwa yoyote katika hali ya dharura ana haki ya kupewa huduma ya kwanza katika hospitali yoyote iliyokaribu bila kujali ni ya binafsi au ya serikali," alisema Dk. Mwaibambe.

 

Alisema huduma kwa mgonjwa yoyote hutolewa bila kujali anauwezo wa kulipia huduma au hana, kwamba sharti hilo limeridhiwa na hospitali zote kabla ya kupewa usajili.

Alibainisha kwa kutoa wito kuwahusu madaktari kwamba kuna umuhimu wa kuhudhuria mikutano ya kitaaluma ya kukumbusha maadili ya udaktari na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa wagonjwa.

Chanzo: ippmedia.com