Dar es Salaam. Takwimu zinaonyesha walemavu 108 hadi 3,016 kati ya 100,000 nchini Tanzania wamepata tatizo hilo kutokana na ugonjwa wa kiharusi.
Hayo yameelezwa leo Jumanne Oktoba 29, 2019 daktari bingwa wa mishipa ya fahamu na ubongo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Patience Njenje wakati akizungumzia maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa kiharusi.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), asilimia 4.5 ya walemavu duniani wanaoshindwa kufanya shughuli zao wamepata hali hiyo baada ya kuugua kiharusi.
Njenje amesema zamani ugonjwa huo ulikuwa unawapata zaidi wenye umri zaidi ya miaka 65, kwa sasa unawatesa hata watoto.
"Pale MNH wanapokea watu kati ya watatu hadi wanne wa kiharusi,” amesema Dk Njenje.
Daktari mwingine, Mohamed Mnacho amesema ni muhimu wananchi kujiwekea utaratibu wa kuchunguza afya zao ili kupambana na ugonjwa huo .
Pia Soma
- Uturuki yaapa kushambulia wapiganaji wa Kikurdi
- MSD mbioni kusaini mkataba usambazaji dawa Sadc
- Dk Shein azindua vitambulisho vya ukazi akieleza umuhimu wake
Amesema dalili za mtoto kuwa ana kiharusi ni kupata degedege, kutumia upande mmoja wa mwili na kushindwa kunyonya au kula.
"Unachotakiwa kufanya ukiona dalili hizi ni kiwahi matibabu," amesema.