Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taharuki mlipuko wa moto jengo la Tanesco

61131 PIC+TANESCO

Mon, 3 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Ubungo jijini Dar es Salaam wamepata taharuki leo mchana Juni 3, 2019 na kutoka ndani ya jengo la makao makuu lililopo Ubungo jijini Dar es Salaam baada ya kuwepo tishio la moto.

Tayari gari mbili za zimamoto zipo kwenye eneo hilo huku gari moja ikiwa karibu na mlango wa kuingilia ndani ili kuzima moto uliojitokeza.

Baadhi ya watu walio kwenye eneo hilo wamesema waliona chumba kimoja kikifuka moshi hali iliyodumu kwa muda mfupi kabla ya moto huo kuzimwa.

Msemaji wa Tanesco aliyepo Dodoma Leila Muhaji amesema taarifa kuhusu tukio hilo zitatolewa baadaye.

Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kinachoendelea

Chanzo: mwananchi.co.tz