Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tahadhari ya serikali juu ya upatikanaji wa dawa muhimu kwenye vituo vya afya nchini

8bdb6ccbad211663b67863b6a4688e6e.jpeg NAIBU katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Gaspa

Sat, 21 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

NAIBU katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Gaspary Muya amewaagiza waganga wakuu wa wilaya zote nchini kuhakikisha dawa muhimu hasa za magonjwa nyemelezi kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi zinapatikana muda wote katika vituo vya afya na zahanati kote nchini.

Naibu huyo anafanya ziara katika mikoa mbalimbali nchini kukagua Konga za vikundi mbalimbali vilivyoanzishwa na watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi WAVIU ili kujiinua kiuchumi na kujenga mushikamano wa pamoja na kutoa hamasa kwa wanachi kupima Afya zao kujitambua na kutumia dawa kwa usahihi.

Katika Ziara yake mkoani Kagera alipata Fursa ya kutembelea Konga za vikundi na kupokea taarifa za vikundi hivyo jinsi walivyojiimarisha kiuchumi lakini Moja ya changamoto alizozipokea Ni malalamiko ya wanavikundi wanaoishi na virusi vya UKIMWI kupitia bima zao zilizoboreshwa CHF hawapati dawa zinazopambana na Magonjwa nyemelezi badala yake wanaandikiwa kununua katika maduka ya dawa Jambo ambalo ni Changamoto kwao.

Kutokana na ziara yake kuambatana na waganga wakuu wa wilaya ametoa wito kuhakikisha kuwa dawa zinazopambana na Magonjwa nyemelezi zinatakiwa kuwepo huku akivihakikishia vikundi hivyo kuwa hospital zote nchini zinaupatikanaji wa dawa kwa asilimia 95 hivyo huenda dawa hizo hazipatikani kutokana na usimamizi hafifu wa wataalamu na uratibu katika maeneo mbalimbali ya kutolea huduma.

Aidha amevipongeza vikundi hivyo ambavyo vinajihusisha na miradi ya kilimo ,ufugaji,kuweka na kukopa Sacoss ,kusaidiana katika shida na Raha na kuwaondoa hofu kuwa serikali iko pamoja nao kupitia vikundi vyao kuhakikisha wanapata dawa kwa asilimia 100 za kufubaza virusi vya UKIMWI pamoja na kuwapatia mikopo ya kuinua Uchumi wao kupitia vikundi vyao.

Ziara ya Naibu katibu mkuu imewashirikisha wadau mbalimbali kwa ajili ya kubeba ajenda ya pamoja na namuna ya Kupambana kupunguza maambukizi mapya kwa asilimia 95 ifikapo 2025 ,pamoja na kutambua changamoto mpya zinazowakabiri watu wanaoishi na Virusi hivyo ,ambapo wadau hao Ni kutoka Time ya Taifa ya kuthibiti UKIMWI TACAIDs, Baraza la Taifa la watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI NACOPHA,Ofisi ya Raisi na serikali za mitaa TAMISEMI na watendaji wa wizara ya Afya.

Hata hivyo ametoa wito kuhakikisha vikundi hivyo vinaeweka nguvu ya ufatiliaji kwa vijana ambapo ametoa takwimu kuwa kwa mwaka 2020/2021asilimia 40 ya maambukizi mapya yalijikita kwa vijana kuanzia miaka 15 Hadi 35 na katika hayo maambukizi asilimia 80 Ni Vijana wa kike na mpaka Sasa Hakuna ufatiliaji mkubwa na uundwaji wa vikundi katika kuwafatilia na kuhakikisha wanafatiliwa kuhusu Afua za lishe , na kuwapa Elimu namna ya kuwakinga wengine hivyo ufatiliaji unahitajika.

Kwa mujibu wa mratibu wa maswala ya UKIMWI mkoani Kagera Issa Malimi alisema kuwa mkoa wa Kagera kiwango Cha maambukizi mapya Ni asilimia 6.5 kwa Sasa kutoka asilimia 4.8 kwa mwaka 2011/2012 huku akitaja changamoto kuwa wanaume wengi hawapendi kupima Afya zao ingawa Kati ya hao wachache wanaopima ndio wenye maambukizi makubwa kuliko wanawake wanaopima.

" Wanawake wanaopima Ni wengi Sana mwaka 2020 wanawake waliofika kituoni kupima Ni 123,951 waliogundulika na maambukizi Ni 7,482 sawa na asilimia 6, wanaume walipima Ni 39,7013 walioathirika Ni 10,136 sawa na asilimia 3.3 hivyo ukilinganisha idadi ya wanawake wanaokuja kupima Ni wengi na wanaume Ni moja ya tatu ya wanawake lakini wanaume ndio wanaokuwa na maambukizi na wote wanatumia dawa na tunanjia za kuwafatilia."alisema Malimi.

Alisema kwa Sasa Kuna mabaraza ya wanaoishi na virusi vya Ukimwi 196 mkoani Kagera ikiwa na jumla ya wanachama 5,950 na vikundi vyao vinauchumi mkubwa na vikundi hivyo vinashirikiana na wahudumu wa Afya Ngazi ya jamii kuhamasisha watu kujitambua ,kutumia dawa na kupinga unyanyapaa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz